Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Magufuli aendelea kusisitiza ugawaji vitambulisho

Magufuli aendelea kusisitiza ugawaji vitambulisho

0 comment 115 views

Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ameendelea kusisitiza ugawaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo ili waweze kujipatia ulinzi na kuacha kunyanyaswa kwa kufukuzwa kila eneo. Rais Magufuli amesema hayo wakati akizungumza na wananchi Mbinga mkoani Ruvuma wakati anaweka jiwe la msingi katika barabara ya Mbinga-Mbamba Bay iliyogharimu Sh. 134.712 bilioni. Hii ni mara ya pili kwa Rais Magufuli kusisitiza suala la vitambulisho tangu kuanza ziara mkoani humo.

“Hadi leo sijapata ripoti yoyote inayoonyesha mkoa au wilaya iliyomaliza kugawa vitambulisho vyake na zimekusanywa kiasi gani cha fedha na kupelekwa TRA. Ungekuwa umeshaniletea ningeshajua ni mkuu wa mkoa gani hataki kufuata maagizo nimtoe au wilaya gani imekaa navyo”. Amesema Rais Magufuli.

katika maelezo yake, amesisitiza kuwa ana mamlaka ya kuwaondoa wakuu wa mikoa na wilaya ambao hawatekelezi zoezi hilo kwa kuwa yeye ndiye aliowachagua.

“Hili nitalifanya, atakayeshindwa kutekeleza maana yake hatekelezi ninayoyataka kuyatekeleza kwa wananchi wadogo. Msinilaumu na nyinyi wananchi chukueni hivi vitambulisho ili mgambo wakija muwaonyeshe, hawatawasumbua. Najua itafika wakati wale wasiokuwa navyo mtasumbuliwa katika maeneo yenu ya biashara, siwatetei mkifukuzwa, kwa sababu mmeyataka wenyewe kwa kutochukua vitambulisho ambavyo ni ulinzi kwenu”. Amesema.

Aidha ametoa onyo kwa wakuu wa wilaya na mikoa wenye tabia ya kutoza fedha zaidi na kulazimisha wajasiriamali kuvinunua.

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter