Home KILIMO Ukosefu masoko, maghala wapoteza mazao

Ukosefu masoko, maghala wapoteza mazao

0 comment 127 views

Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli amesema kuwa takribani asilimia 40 ya mazao yote ambayo huzalishwa na wakulima hapa nchini hupotea kutokana na ukosefu wa masoko pamoja na maghala. Rais Magufuli amesema hayo mkoani Ruvuma alipokuwa akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali kutoka serikalini wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha usindikaji mahindi cha Mlale JKT.

Rais Mgufuli amesema mbali na kiwanda hicho kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali kufikia uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda, kwa kiasi kikubwa pia kitasaidia kupunguza changamoto hiyo. Imeelezwa kuwa kiwanda hicho ambacho kimegharimu Sh. 444.77 milioni kinatarajia kusindika tani 440 za mahindi, kuzalisha tani 308 za unga wa sembe na tani 132 za pumba.

Pamoja na hayo, Rais Magufuli ametumia nafasi hiyo kupongeza Jeshi la Wananchi (JWTZ) na Jeshi la Kulinda Taifa (JKT) kwa harakati zao za kulinda taifa na kudumisha hali ya amani,

“Jeshi letu la Wananchi linafanya kazi nzuri sana katika sekta mbalimbali za ujenzi na hata viwanda, nawapongeza sana”. Amesema Rais Magufuli.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter