Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa ameitaka Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini (TCDC) kwa kushirikiana na Bodi za Mazao kuweka mikakati ambayo itamsaidia mkulima kuongeza mauzo na uzalishaji wa mazao.
“Hakikisheni mnakuwa na mkakati wa pamoja na upatikanaji wa pembejeo na uhakika wa masoko na namna bora ya kuhifadhi mazao ya wakulima ikiwemo ujenzi wa maghala. Tumeona juhudi zinazofanywa na serikali katika katika kumsaidia mkulima kunufaika na shughuli zake za kilimo kupitia sekta ya ushirika na mabadiliko kwa baadhi ya maeneo japo kuwa bado kuna changamoto”. Amesema Naibu Waziri huyo.
Bashungwa amesema sio jukumu la viongozi wa juu kutafuta masoko kwa ajili ya wakulima, hivyo kuitaka TCDC na Bodi ya mazao kuwatafutia masoko wakulima ndani na vilevile nje ya nchi, huku akisisitiza kuwa jambo hilo linawezekana endapo mfumo wa ushirika utatumika vizuri.
Naye, Mwenyekiti wa TCDC, Dk. Titus Kamani amesema mkutano huo umelenga kutafsiri ujenzi wa uchumi katika sekta ya kilimo na kujadili namna ya kutatua migogoro katika sekta hiyo na kuhakikisha haijitokezi tena.
“Tumeona juhudi zinazofanywa na serikali katika kumsaidia mkulima kunufaika na shughuli zake za kilimo kupitia sekta ya ushirika na mabadiliko kwa baadhi ya maeneo japo kuwa bado kuna changamoto”. Amesema Dk. Kimani.