Home KILIMO Serikali yapiga marufuku usafirishaji wa mpunga Kilombero

Serikali yapiga marufuku usafirishaji wa mpunga Kilombero

0 comment 42 views
Na Mwandishi wetu

Baada ya kufanya mazungumzo na wadau wa kilimo cha mpunga kutoka wilaya za Kilombero, Mvomero, Ulanga na Malinyi kwa kushirikiana na taasisi za kusaidia kilimo cha zao hilo, Mkuu wa mkoa wa Kilombero James Ihunjo amesema serikali imepiga marufuku usafirishaji wa mpunga kutoka wilayani Kilombero kwenda maeneo mengine.

Ihunjo amedai kuwa kupiga marufuku usafirishaji wa mpunga kunalenga kuwapa uwezo wakulima kunufaika na kilimo chao hali itakayowakwamua kiuchumi na kuwaondoa katika umaskini.

Mkuu huyo wa wilaya pia amesema wafanyabiashara watakaokaidi agizo hilo watawajibishwa kwa mujibu wa sheria huku akisisitiza kuwa mpunga unaouzwa ni lazima uchakatwe ili kuongeza thamani ya zao hilo, jambo ambalo litamfaidisha mkulima.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter