Home BIASHARA Serikali yaruhusu biashara vyuma chakavu

Serikali yaruhusu biashara vyuma chakavu

0 comment 121 views

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amesema serikali imeruhusu biashara ya taka hatarishi, ikiwa ni pamoja na vyuma chakavu kwa wafanyabiashara wenye leseni na ambao wamekaguliwa na Baraza la Usimamizi wa Mazingira Tanzania (NEMC) pamoja na kupewa cheti cha ukaguzi, ambapo wafanyabiashara hao watatakiwa kufuata taratibu na kanuni mpya.

Makamba amesema baada ya serikali kupitia maoni ya wadau mbalimbali, kanuni zijazo zitatenganisha ada za wakusanyaji, wauzaji, wasafirishaji na wamiliki wa viwanda huku wakizingatia mporomoko wa bei za bidhaa.

“Katika kipindi hiki cha mpito tutazunguka kuongea na watu mahususi wataangalia vibali na iwapo itabainika mtu hajakaguliwa na kupewa cheti cha EAA ajue moja kwa moja atafungiwa kufanya biashara hiyo, hata zikija kanuni mpya asiombe leseni”. Amesema Waziri Makamba.

Pamoja na hayo, pia ameeleza kuwa sababu ya kufanya mabadiliko kwenye kanuni  za usafirishaji wa taka hatarishi nje ya nchi ilitokana na wasafirishaji wengi kusafirisha taka ambazo zingeweza kutumika kama malighafi ya nondo nchini.

“Kuanzia Januari hadi sasa kontena 280 yaani kilo milioni tano za chuma chakavu zimetoka Tanzania kwenda nje, na zinazoingia pia ni nyingi, na hizo ni zilizorekodiwa pekee inaonyesha ni kiasi gani nchi inapoteza malighafi ambayo ingetumika nchini na mapato pia”. Amesema.

Kwa upande wao, wafanyabiashara wa vyuma chakavu wameiomba serikali kuwapatia vitambulisho kutokana na mitaji yao kutozidi Sh. milioni 3.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter