Home FEDHA Dodoma, Arusha vinara ukusanyaji mapato

Dodoma, Arusha vinara ukusanyaji mapato

0 comment 31 views

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amesema kuwa mikoa ya Arusha na Dodoma zimeibuka vinara katika kukusanya mapato ya ndani kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2018/2019. Jafo amesema hayo wakati akitoa taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri na kueleza kuwa, halmashauri ya jiji la Dodoma imeongoza kwa kukusanya mapato ghafi kuliko halmashauri zote nchini na imefanikiwa kukusanya kiasi cha Sh. 14.4 bilioni kati ya bajeti yao ya kukusanya Sh. 68.6 bilioni, ikiwa ni sawa na asilimia 21 ya  malengo waliyojiwekea.

Jiji la Arusha linaongoza kwa kukusanya vizuri kiasilimia na imefanikiwa kukusanya asilimia 26 ya malengo waliyojiwekea ikiwa imekusanya kiasi cha Sh. 4.1 bilioni kati ya Sh. 15.6 bilioni ya malengo kwa mwaka wa fedha 2018/19.

“Ieleweke wazi kuwa Jiji la Arusha ndio lililofanya vizuri kimakusanyo kwa mujibu wa asilimia lakini jiji la Dodoma ndio lililokusanya fedha nyingi zaidi kuliko halmashauri zote Tanzania”. Ameeleza Waziri huyo.

Kwa mwaka wa fedha 2018/2019, halmashauri zilipangiwa kukusanya Sh. 735.6 bilioni kutoka vyanzo vya ndani na hadi Septemba 30 mwaka huu, halmashauri zilikusanya jumla ya Sh. 143.6 bilioni  sawa na asilimia 20 ya makisio ya mwaka.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter