Home VIWANDAUZALISHAJI Makamba: Tutakabiliana na mifuko ya plastiki

Makamba: Tutakabiliana na mifuko ya plastiki

0 comment 115 views

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba amesema zuio la mifuko ya plastiki nchini limelenga kulinda afya za wananchi na mazingira.

“Madhara yanayotokana na mifuko hiyo ni makubwa sana hivyo si rahisi kwa mtu kuona katika hali ya kawaida. Katika kukabiliana na zuio hili, changamoto ni nyingi ikiwemo kutokuwa na ufahamu mpana wa wananchi juu ya athari zake lakini tumejipanga kuhakikisha linafanikiwa na hatua muhimu zaidi ni kutoa elimu kwa wananchi. Katazo la kitu kama hiki halikosi vikwazo, kelele na hata vitisho kutoka kwa watumiaji na wazalishaji. Hivyo tumejipanga kukabiliana na yote hayo”. Amesema Waziri Makamba.

Pamoja na hayo, ameongeza kuwa licha ya Wizara hiyo kuhakikisha zuio hilo linafanikiwa, elimu inatakiwa kutolewa kwa wananchi kuhusu madhara ya mifuko hiyo na matumizi ya mifuko mbadala.

“Tumejipanga kiasi cha kutosha juu ya namna ya kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza na jambo muhimu sana ni ushirikiano kwa kuwa mazingira ni zuala muhimu kwa kizazi cha leo na kesho, hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuyalinda”. Amesema Makamba.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter