Home VIWANDAMIUNDOMBINU ATCL mbioni kuongeza ndege

ATCL mbioni kuongeza ndege

0 comment 107 views

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amesema ndege mbili aina ya Bombardier D8 Q400 na Boeing B787-8 Dreamliner zinatarajiwa kuletwa nchini mwishoni mwa mwaka huu. Ameyasema hayo bungeni Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Khadija Nassir Ali ambaye amehoji kama serikali inaendelea na ununuzi wa ndege, haioni ni wakati muafaka kuhakikisha ndege hizo zinakwenda kila mkoa wenye kiwanja na nchi jirani kusaidia kushusha gharama za usafiri?

Naibu Waziri huyo ameeleza kuwa kupitia ujio wa ndege hizo, Shirika la ATCL litaweza kutoa huduma ya kutosha.

“Uwapo wa ndege mpya za kutosha utaiwezesha ATCL kuhimili ushindani wa kibiashara katika utoaji huduma za usafiri wa anga katika masoko ya ndani, kikanda na kimataifa”. Amesema Nditiye.

Akizungumzia usafiri wa anga katika kila mkoa nchini, Nditiye amesema utekelezaji wake upo ndani ya mkakati wa miaka mitano wa ATCL, na mpango wa biashara ambao huandaliwa kila mwaka.

Aidha ametaja mikoa tisa ambayo ATCL inasafirisha abiria kuwa ni pamoja na Dodoma, Mwanza, Kagera, Kigoma, Mbeya, Kilimanjaro, Zanzibar, Tabora na Mtwara. Nchi tano ambazo ATCL inatoa huduma kwa sasa ni Hahaya (Morocco), Harare (Zimbabwe), Bujumbura (Burundi), Entebbe (Uganda), na Lusaka (Zambia).

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter