Home VIWANDANISHATI Kalemani ahamasisha umeme vijijini

Kalemani ahamasisha umeme vijijini

0 comment 105 views

Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani ametoa agizo kwa Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kukamilisha zoezi la uwekaji wa umeme katika vijiji nane vilivyopo katika wilaya ya Mpwapwa. Hadi sasa vijiji 48 kati ya 57 vimefikiwa na huduma ya umeme wilayani humo, na serikali imelenga kukamilisha zoezi hilo hadi ifikapo Disemba mwaka huu.

Wakati wa ziara hiyo, Dk. Kalemani amewasha umeme katika zahanati ya Igogi One, na kumsisitizia Meneja wa Tanesco kuendelea na zoezi la uwekaji wa umeme kwenye makazi ya wananchi, huku akiagiza ujenzi wa vituo vidogo vya umeme kila kijiji ili kuepusha changamoto ya huduma kutoka katika shirika hilo.

Kalemani amesema umeme ni biashara na kugawa Umeme Tayaru (UMETA) 280 kwa wanakijiji wa Igogi One. Pia Waziri huyo ameagiza mkandarasi wa kampuni ya OK kukamatwa kutokana na kushindwa kutekeleza uwashaji wa umeme katika kijiji cha Chibwegere uliotakiwa kukamilika mwaka jana.

Naye Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene ametoa shukrani kwa Waziri huyo kwa kupeleka umeme kijijini hapo na kuwataka wanakijiji ambao bado hawajapata umeme kuwa na subira.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter