Home BIASHARAUWEKEZAJI Fursa kwa wafanyabiashara wa China

Fursa kwa wafanyabiashara wa China

0 comment 159 views

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki ametoa wito kwa wafanyabiashara wa China kuwekeza katika usindikaji wa mazao ya chakula na kutumia malighafi zinazopatikana nchini ili kukidhi mahitaji ya soko itakapofika mwaka 2050.

Kairuki ametoa wito huo wakati akifungua kongamano la uwekezaji kati ya China na Tanzania katika kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) ambapo ameeleza kuwa hadi kufika mwaka 2050, kutakuwa na mahitaji makubwa ya chakula kutokana na watu wengi wa vijijini kukimbilia mijini kwa ajili ya kutafuta kazi za viwandani na huduma.

Pia ameongeza kuwa Tanzania ni nchi yenye rutuba na maji ya kutosha hivyo kurahisisha uzalishaji wa mazao yanayotumika zaidi barani Afrika zikiwemo nafaka, maharage, mihogo, viazi vitamu na matunda ya aina mbalimbali kama parachichi.

“Tanzania ina kila kitu na hamtohitaji kuleta mazao kutoka nje kwani kwa ardhi iliyopo na maji kuna uwezekano mkubwa wa kulisha kwa chakula majirani zetu kutokana na mahitaji yaliyopo. Lazima uwekezaji wenu ujikite katika viwanda, lakini kubwa kwa kutumia malighafi zinazopatikana hapa nchini”. Ameeleza Kairuki.

Aidha, amesema kuwa Tanzania ina soko la uhakika kutokana na uanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambayo ina watu milioni 152 pamoja na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambayo ina watu milioni 800.

Pamoja na hayo, Waziri huyo amebainisha kuwa biashara kati ya China na Tanzania imekua kutoka Dola za Marekani bilioni 3.9 hadi bilioni 7 kufikIa mwaka jana.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter