• Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
Sunday, June 26, 2022
  • Login
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
No Result
View All Result

Kampuni za utalii zifanye hivi kuvutia wateja

Ni vyema kutengeneza mbinu mpya ili kuhamasisha zaidi utalii wa ndani.

Leah Nyudike by Leah Nyudike
August 21, 2019
in BIASHARA
0
Kampuni za utalii zifanye hivi kuvutia wateja
Share on FacebookShare on Twitter

Utalii ni moja ya sekta yenye mchango mkubwa katika uchumi wa Tanzania. Kupitia sekta hii watanzania na raia kutoka nje ya nchi wamenufaika kwa kuanzisha biashara mbalimbali zinazohusiana na masuala ya utalii. Moja ya biashara ambayo inashika kasi ni kuandaa safari kwa ajili ya watalii kwenda kutembelea maeneo mbalimbali nchini.

Kampuni zinazojihusisha na uandaaji wa safari hizi zinatakiwa kuongeza juhudi zaidi hata baada ya kujipatia mafanikio ili kuweza kusonga mbele zaidi kwani kila siku mawakala wapya wanaanzisha biashara hii.

Hizi ni baadhi ya mbinu ambazo kampuni inaweza kutumia ili kupata wateja zaidi na kuongezana kuwahamasisha watalii kutoka maeneo mbalimbali kutumia huduma zao pindi wanapokuja kutembea nchini:

Siku zote biashara huanzishwa baada ya kuona mapungufu yaliyopo katika jamii. Ili kupata mauzo zaidi unatakiwa kuwaonyesha wateja faida za kutumia huduma katika kampuni yako. Badala ya kutumia muda mwingi kushindana na washindani wako, jikite katika kutoa huduma za kipekee ambazo zitawahamasisha wateja kurudi tena. Kwa mfano unaweza kuwahamasisha wateja kutoa ushuhuda katika tovuti yako au mitandao ya kijamii ili kuwavutia wateja wapya kwa sababu watu husoma maoni ya watu wengine mtandaoni kabla ya kufanya maamuzi hiyo ushuhuda ni nafasi nzuri ya kushawishi wateja wapya.

Mitandao ya kijamii ni muhimu katika biashara hii. Watalii wengi hutumia mtandao hivyo tumia fursa hiyo kuwasiliana na wateja wako kwa kuweka picha, video, kuuliza maswali katika akaunti yako ili kuwajulisha wateja wako wa zamani na wapya kuhusu huduma zilizopo. Watalii huhamasika kujaribu vitu vipya kutokana na taarifa zinazowekwa katika mtandao

ADVERTISEMENT

Watalii hufurahishwa na huduma maalum. Kama kampuni, inatakiwa kujiongeza na kujua ni vitu gani vinaweza kuwavutia wateja wako. Kwa mfano ikiwa unajua watalii hupendelea kutembea na kuona mandhari inayowazunguka, unaweza kuwapa darubini bila kuwatoza fedha. Hivi ni vitu vidogo lakini mara nyingi maana yake kwao inakuwa kubwa. Ni muhimu kuhakikisha wateja wako hawasahau uzoefu waliopata kwako.

Jitahidi kushirikiana na makampuni mengine ya kitalii ikiwa ni pamoja na hoteli, migahawa, sehemu za maonyesho ili kuwarahisishia wateja kupata huduma zote muhimu na kuepuka kuhangaika. Tengeneza vifurushi vya kuvutia, rahisi kuelewa na katika bei rafiki. Epuka kutoza fedha nyingi kwani inaweza kuwa chanzo cha kukosa wateja. Kwa mfano unaweza kuweka vifurushi vya bei ya chini ambavyo vinaruhusu marafiki kadhaa kuchangia fedha na kutembelea vivutio kama Serengeti, Zanzibar nk. Hii itawahamasisha wengine wengi kujipanga na kulipia kifurushi hicho.

Kitu kimoja ambacho mawakala wa utalii wanatakiwa kufanyia kazi ni masuala ya bei kati ya watalii wa ndani na nje. Ni rahisi kwa watalii kutoka nje kulipia kiasi chochote lakini kwa upande wa watalii wa ndani, ni watu wachache wapo tayari kutumia gharama kubwa kujionea vivutio vilivyopo. Inaweza kuwa ni bei ya kawaida, lakini ili kuwahamasisha watalii wa ndani, ni vizuri kwa wahusika kuja na mbinu mpya ambazo zitawashawishi watanzania wengi zaidi kutembelea maeneo hayo.

 

Tags: fedhaSerengetiTanzaniauchumiutaliiwatejazanzibar
Leah Nyudike

Leah Nyudike

Mwandishi

Next Post
Programu ya 'Worknasi' ichangamkiwe

'Worknasi' ichangamkiwe

Discussion about this post

Habari Mpya

Miamala ya simu yaongeza Pato la Taifa

June 24, 2022

Mapendekezo bima ya afya kwa wote

June 23, 2022

Kilimo biashara, sekta yenye fursa za uwekezaji

June 23, 2022

Turkish Airlines yarejesha safari zake KIA

June 22, 2022
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla akizungumza katika warsha ya viongozi wa Serikali wa mkoa na Bank ya NMB.

Benki ya NMB yapongezwa

June 22, 2022

Rais Samia azindua taasisi Zanzibar

June 20, 2022

KUHUSU SISI

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905. PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.

LATEST

Miamala ya simu yaongeza Pato la Taifa

by Pesatu Reporter
June 24, 2022
0

Miamala ya fedha kwa njia ya simu imechangia kuongezeka kwa pato la Taifa kutoka asilimia 40 mwaka 2013 hadi kufikia...

Mapendekezo bima ya afya kwa wote

by Pesatu Reporter
June 23, 2022
0

Mapendekezo yamepitishwa kwa kila Mtanzania kuwa na bima ya afya. Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM (NEC) leo 23...

RECOMMENDED

Waziri Mwijange aja na orodha ya viwanda visivyofanya kazi

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

  Na Mwandishi wetu. Baada ya Rais John Magufuli kuonyesha kukerwa na kitendo cha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji...

Nane Nane itumike kama darasa huru kwa wakulima

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

Na Mwandishi wetu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejitolea kuwapa mafunzo ya siku moja wakulima mkoani Lindi...

No Result
View All Result
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI

© 2022 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In