Home AJIRA Jiajiri na Uber sasa

Jiajiri na Uber sasa

0 comment 124 views

Biashara ya Uber inafahamika sana jijini Dar es salaam kwa Tanzania. Huduma hii inamuhitaji mtumiaji (dereva au mteja) kuwa na smartphone, simu ambazo zinatumiwa sana hivi sasa. Ptrogramu hii pia ni rahisi kutumia, na bei zao ni nafuu kulingana na muda na foleni za barabarani.

Uber ni nini?

Ni programu ya kisasa ambayo humuunganisha dereva-washirika na mteja. ambapo mshirika-dereva hutumia gari lake au gari la mtu aliyemuajiri (partner) kwa ajili ya kuwafuata wateja katika sehemu husika na kuwapeleka sehemu wanayotaka. Dereva hulipwa baada ya kukamilisha kila safari aidha kwa fedha taslimu au kwa njia ya benki ambapo fedha hizo baada ya washirika kukata asilimia chache hutumia siku kadhaa kumfikia dereva kwenye akaunti yake.

Faida ya kujiajiri na Uber

Ukijiajiri na Uber kwanza inakuwa rahisi kufanya shughuli nyingine kwa sababu kampuni ya Uber inamruhusu dereva kufanya biashara muda wowote lakini kwa masaa kumi na mbili. Hivyo kama una gari yako na unafanya kazi katika kampuni hiyo unaweza kufanya kazi zako nyingine na muda ambao unakuwa huna kazi unaweza kufanya ‘route’ za Uber kujipatia kipato zaidi.

Kwenye suala la usalama, dereva anakuwa na uhakika wa usalama akiwa anafanya kazi yake. Programu ya Uber huonyesha safari nzima inavyokwenda. Mbali na hilo, pia Uber wameanzisha mfumo (kitufe ambacho dereva ana uwezo wa kubonyeza ndani ya gari) ambao unamuwezesha dereva kutoa saini kama mteja anafanya jambo linalomfanya asijisikie vizuri au salama.

Dereva ana uwezo wa kuchagua safari. Kupitia programu ya Uber dereva anaweza kuangalia safari ipi anaweza kuifanya na ipi hatoweza kuifanya. Hivyo ni rahisi kujua safari ipi itamuingizia fedha zaidi na muda ambao atachukua kukamilisha safari hiyo.

Kwa ujumla, kujiajiri kupitia usafiri wa Uber humsaidia dereva kufanya kazi kwa bidii, kwa sababu mteja ana uwezo wa kutoa maoni kuhusu safari katika programu hiyo. Ikitokea wateja wengi wanalalamika kuhusu dereva mmoja, dereva huyo atapata changamoto zinazoweza kusababishwa kuachishwa kazi. Kama mtu anataka kujipatia kipato cha ziada na amedhamiria kufanya kazi kwa bidii basi biashara ya uber inamfaa.

Uvumilivu katika biashara hii ni muhimu. Dereva hukutana na wateja aina mbalimbali na kuna muda bei za safari hushuka sana na kuondoa matumaini kwa dereva kutokana na fedha kidogo anazopata. Ni muhimu kwa dereva kuwa mvumilivu kipindi bei inapopanda na kushuka.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter