Home KILIMO Majaliwa aagiza umakini zaidi kwenye zao la tumbaku

Majaliwa aagiza umakini zaidi kwenye zao la tumbaku

0 comment 168 views
Na Mwandishi wetu

Maofisa Kilimo na Maofisa Ushirika mkoani Tabora wametakiwa kusimamia kwa makini ukuaji wa zao la Tumbaku kuanzia msimu ujao. Agizo hilo limetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa  akifanya ziara mkoani humo.

Waziri Majaliwa amewataka watumishi kutoka idara za kilimo kutumia vyombo vya habari kutoka ndani na nje ya nchi kuelezea mikakati ya serikali katika jitihada za kuinua zao hilo. Kabla hajaondoka mkoani humo, Majaliwa ametaka watumishi hao kuwa na mazungumzo na wakulima wa zao hilo ili waweze kubadilishana mfumo na kuwainua kibiashara.

Pia Bodi ya Tumbaku itakayoundwa ijipange kulinda maslahi ya mkulima. Waziri Mkuu amesema ili kuongeza ufanisi kwenye zao la tumbaku inabidi baadhi ya majukumu yapunguzwe kwenye bodi hiyo ambayo makao yake makuu ni Tabora.

Bodi hiyo pia itashirikiana na vyuo vya utafiti ili kuhakikisha mbegu bora zenye uwezo wa kustahimili hali ya hewa na magonjwa zinapatikana. Naye Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Tabora Hassan Wakasuvi ametoa shukrani kwa Waziri Mkuu kwa ziara yake ya siku nne katika mkoa huo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter