Home BIASHARA Jinsi ya kupata leseni ya biashara

Jinsi ya kupata leseni ya biashara

0 comment 156 views

Leseni ya biashara ni muhimu kwa mfanyabiashara kwa sababu ni utambulisho kuwa biashara hiyo ni halali na inatambulika serikalini. Mara nyingi huwa haichukui muda mrefu kupata leseni hiyo ili mradi mfanyabiashara awe ameambatanisha nyaraka zote muhimu kama ilivyoelekezwa.

Leseni za biashara hutolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) na katika halmashauri zote nchini. Kama biashara yako ina mtaji mkubwa, unashauriwa kuchukua leseni yako moja kwa moja Brela na ikiwa biashara yako ni ya kawaida kwa mfano, viwanda vidogo, uuzaji wa bidhaa za jumla na rejareja unaweza kujipatia leseni yako katika halmashauri yako, Brela au katika wilaya yako kama inavyoelezwa katika kifungu cha Sheria cha 11(1) cha Sheria ya leseni za biashara namba 25 ya 1972 .

Zifuatazo ni nyaraka ambazo mfanyabiashara anatakiwa kuambatanisha ili kupata leseni ya biashara:

  • Nakala ya hati ya kuandikisha jina la Biashara au Kampuni (Photocopy of Certificate of Incorporation or Registration & Extract)
  • “Memorandum, and Articles of Association” ambazo zitaonyesha kuwa kampuni imeruhusiwa kisheria kufanya biashara inayoombwa, pamoja na majina ya wamiliki wa kampuni hiyo, pamoja na hisa zao na utaifa wao
  • Uthibitisho wa uraia kwa kuwasilisha, nakala ya hati ya kusafiri nje ya nchi ya Tanzania au hati ya kusafiri katika nchi za Afrika Mashariki, cheti cha kuzaliwa au hati ya kiapo (Affidavit) kuonyesha kuwa ni mtanzania, na kama mgeni alete hati ya kuishi nchini daraja la kwanza (Residence Permit Class A).
  • Endapo wenye hisa wote wapo nje ya nchi itabidi maombi yaambatane na hati ya kiwakili (Power of Attorney) ya kumpa mamlaka raia wa Tanzania, raia wa kigeni mwenye hati ya kuishi nchini daraja “A” au hati ya kufanya kazi nchini daraja “B” zinazoainisha kuwa anasimamia kampuni husika.
  • Nakala ya ushahidi wa maandishi kuwa ana mahali pa kufanyia biashara (lease agreement, Title deed, Certificate of occupancy e.t.c)
  • Hati ya kujiandikisha kama mlipa kodi (Tax Payer Identification Number – TIN)

Baada ya kuwa na nyaraka hizo, mfanyabiashara hutakiwa kujaza fomu ya maombi ya leseni (TFN 211 ya mwaka 2004) na kuambatanisha nyaraka zote kwa ajili ya kukufanyiwa ukaguzi na kujulishwa kiasi cha fedha (ada) ambacho anatakiwa kulipa.

Kwa mfano kwa biashara yenye mtaji mkubwa malipo hufanyika katika benki ya CRDB katika tawi lolote katika Akaunti namba: Namba 0150413356300; Jina Revenue Collection Trading Licence – MIT. Baada ya malipo mfanyabiashara hutakiwa kuwasilisha kielelezo kwamba ameshalipia benki ili kupata risiti halali ya serikali.

Itambulike kuwa kila biashara huwa na malipo ya aina yake, na kitendo cha kumiliki leseni ya biashara humsaidia mfanyabiashara kuepukana na changamoto ya kufungiwa biashara kila wakati pia huwa rahisi kupata mikopo kutokana na uhalali wa biashara yake.

Aidha mfanyabiashara ana uwezo wa kumiliki leseni ya biashara zaidi ya moja ili mradi kama kila leseni inatumiwa katika biashara husika.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter