Home BIASHARA Makamba atoa onyo kwa watendaji

Makamba atoa onyo kwa watendaji

0 comment 112 views

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba amewaagiza watendaji wa mkoa wa Dar es salaam kutotumia nguvu kwa wananchi watakaokutwa na mifuko ya plastiki kuanzia tarehe 1 Juni mwaka huu.

Makamba ametoa agizo hilo wakati akizungumza na watendaji wa mkoa wa Dar es salaam wakiwemo wakuu wa wilaya, makatibu tawala, wakurugenzi, madiwani, wenyeviti na watendaji wa kata na mitaa, wasimamizi wa masoko, maofisa afya, mazingira na biashara.

“Katika utekelezaji wa Sheria hii mpya inayoanza Juni Mosi mwaka huu, hatutegemei kuona watu wanaendelea kubeba mifuko, lakini pia hatutegemei kuona kina mama wanapigwa virungu na mgambo kisa wamebeba mifuko na wala hatutegemei kuona watu kuporwa mali zao. Tunatarajia hakuna mwananchi ambaye atatumia mifuko ya plastiki kuanzia Juni Mosi, lakini watendaji wanaosimamia kazi hii, hatutarajii kuona wanapita kwenye maofisi, maduka na kufungua kwenye magari ya watu kutafuta mizigo ya mifuko hii hatutarajii kabisa”. Amesema Makamba

Licha ya  mpango wa kuendelea kutoa elimu kuhusu udhibiti wa matumizi ya mifuko hiyo kwa jamii, Waziri huyo amesema atakayekutwa na mifuko hiyo atawajibishwa kisheria.

“Tutatumia muda mrefu kuendelea kuelimishana na kuelekezana kuhusu kuacha matumizi ya mifuko hii ya plastiki, hivyo utekelezaji wake hatutegemei ukitumika kuwanyanyasa watu na kupora mali zao” amebainisha hilo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter