Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Hatua 5 muhimu kwa wanawake wajasiriamali

Hatua 5 muhimu kwa wanawake wajasiriamali

0 comment 121 views

Mara nyingi huwa nahamasishwa na kujitoa na ujasiri wa wanawake wajasiriamali. Wanawake huanzisha biashara zao kwa sababu mbalimbali. Kwa mujibu wa Utafiti wa SCORE wanawake wa rika mara nyingi huendeshwa na fursa ya soko huku watu wazima huendeshwa na mahitaji.

Lakini bila kujali umri au msingi wa mambo yanayowaendesha, kuna mambo ya kuzingatia ambayo yanatakiwa kutumika kwa wanawake wajasiriamali wote ikiwa wanajiandaa kuanzisha biashara.

  • Jitahidi kwa uaminifu

Ujasiriamali si sahihi kwa kila mtu, so ni muhimu kuamua kama utakufaa- kabla hujatumia kiasi kikubwa cha muda, fedha, jasho, na machozi kuanzisha biashara.

Wamiliki wa biashara wanatakiwa kuwa waanzishaji ambao hawasubirii watu wengine kufanya maamuzi. Je unahamasika? Una uwezo wa kufanya maamuzi? Pia wanatakiwa kuwa na urahisi wa kuchukua kiwango fulani cha hatari. Mafanikio katika biashara huwa si asilimia mia moja. Je unaweza kukabiliana na hatari na kutokuwa na uhakika? Je unaweza kushughulikia vikwazo na kukataliwa bila kukata tamaa?

Wajasiriamali wanatakiwa kuwa na uwezo wa kusimamia muda na kuweka vipaumbele kwa ufanisi. Je unaweza kupangilia mambo na kuweza kutambua kazi zinazohitaji tahadhari ya haraka dhidi ya zile zinazoweza kusubiri?

  • Fikiria jinsi ujasiriamali utakavyoathiri mahusiano binafsi

Kuanzisha biashara kunahitaji muda na uzingatiaji-mara nyingi kwa kiasi kikubwa kwa yote. Tambua kuwa hili litakuwa na athari kwa kiasi fulani kwa katika uhusiano na mpenzi wako, watoto, ndugu wengine na marafiki. Watu wanaweza kujisikia vibaya kutokana na muda na tahathari uliyowekeza katika uanzilishi wako na si kila saa wataelewa kwanini huwezi kutenga muda wa saa moja kwaajili ya kuwasiliana nao, kupata nao chakula cha mchana, au kufurahia nao kwa ujumla.

Mwenzi wako na watoto wanaweza kujisikia vibaya ikiwa wanahitaji ufanye mambo zaidi nyumbani kama ilivyozoeleka. Ni muhimu kuwasiliana na kuweka matarajio tangu mwanzo ili uweze kuzuia hisia ngumu na kudumisha uhusiano mzuri.

  • Tarajia jinsi itakavyoathiri maisha yako mwanzoni

Kuanzisha biashara huhitaji kupunguza baadhi ya anasa za maisha. Nikisema anasa simaanishi caviar, safari za kigeni, mikoba ya kubuni- huenda unahitaji muda wa kuacha vitu ambavyo hufurahia mara kwa mara kwamfano, kwenda kula mgahawani, kukununua kifurushi cha bei cha television nk je unaweza kukubaliana na hilo?je  familia yako inaweza kukubali hilo?

  • Jifunze unachohitajika kujifunza

Ujasiriamali ni safari inayoambatana na uzoefu pamoja na elimu. Ukishapita mchakato wa kuanzisha biashara na kuiendesha, utaona mapungufu katika ujuzi wako na uwezouliokuwa haujui kabla.

Kuwa na ufahamu na kubali kwamba wewe si mkamilifu na utafanya makosa. Jambo la muhimu ni jinsi utakavyoweza kuchukulia na kukabliana na changamoto hizo. Weka kando kiburi na uwe na nia ya kujifunza na kjiboresha.

  • Jiamini

Maneno yangu ya mwisho ya ushauri: Jiamini wewe na uwezo wako. Sherekea na kuimarisha uwezo wako binafsi. Zaidi ya hayo, jifunze kutofautisha kati ya upinzani unaojenga  maneno yasiyo na nia nzuri wakati unapokea maoni kutoka kwa wengine. Kwanza itakusaidia kuwa mjasiriamali mwenye nguvu zaidi, na kukupa msukumo zaidi wa kujiamini ikiwa hautopeleka moyoni kila kitu unachoambiwa.

“Wanawake wote ni nguvu za asili, na ninaamini nguvu zao.” – Stephanie McMahon. Kuanza biashara si rahisi, lakini ikiwa unafanya bidii , kwa uwezo wako, kujiandaa kwa changamoto, na kufuatilia rasilimali kwa busara, unaweza na utafanikiwa.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter