Home BIASHARA Fursa kubwa za biashara Afrika 2019

Fursa kubwa za biashara Afrika 2019

0 comment 100 views

Fursa hutokana na matatizo au ukosefu wa bidhaa au huduma fulani katika jamii. Na ndio maana kila siku tunaona watu mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali duniani wanakuja kuwekeza Afrika kwa sababu wanaona kuna fursa nyingi.

Zamani masuala ya uwekezaji barani  Afrika yalikuwa yanachangamkiwa zaidi na watu wa mabara mengine  kuliko waafrika wenyewe. Hali hiyo imebadilika sana, sasa hivi waafrika wamejikita katika uwekezaji, ujasiriamali, biashara ndani na nje ya nchi, ni jambo zuri kuona waafrika wanafanikiwa hadi kimataifa kwani kwa hali hiyo umasikini nao unapungua, na maendeleo yanafanyika kuanzia ngazi ya familia, kata, wilaya, mji, nchi na hata bara zima.

Hizi ni baadhi ya fursa za biashara barani Afrika kwa mwaka 2019:

Bidhaa za chakula za kiafrika za kuuza nje

Ni kawaida kuona malighafi zinazopatikana barani afrika zinaenda kuuzwa nje ya bara, hivyo wazalishaji huuza malighafi hizo kwa hasara hivyo kutofaidika na kazi wanazofanya kwa bidii. Lakini hali hiyo imeanza kubadilika kwani sasa wafanyabiashara mbalimbali wameamua kuchukua fursa ya kubadilisha malighafi kuwa bidhaa na kuzipeleka katika soko ya nje kwa bei nzuri, hali inayoleta matumaini kwa sababu wanapata faida zaidi.

Inaelezwa kuwa FairAfric imejikita katika kuuza chocolate zinazoitwa ‘Made in Africa Organi chocolate ambazo zinatengenezwa na kakao kutoka Ghana na kuuzwa Ulaya. Kwa mwaka 2018 walisafirisha bidhaa zaidi ya 250,000 na kupata Euro 50,000.

Pia Garden Coffee ni moja ya kampuni inayokuwa kutoka Ethiopia ikiwa inajihusishwa na kahawa na kusafirisha katika nchi zaidi ya 20 ikiwa ni pamoja na Urusi, Sweden, Ujerumani na Marekani.

Mitindo na nguo

Tasnia ya mitindo ni kubwa sana duniani. Imekuwa kawaida kuona watu wakifurahia nguo zinazotoka nje ya nchi kuliko zinazotengenezwa barani Afrika. Lakini hadi sasa jambo hilo limekuwa likiendelea kubadilika kwani wanamitindo mbalimbali wameamua kuwahamasisha watu kununua zaidi bidhaa za nguo zinatengenezwa hapa kwa kutengeneza nguo nzuri, zinazoenda na wakati na kwa bei nzuri.

Hata baadhi ya makampuni kutoka nje kama H&M na Primark wanatoa malighafi zao barani Afrika hivyo kuwanufaisha wazalishaji wa malighafi za kutengenezea nguo. Pia wanamitindo mbalimbali kutoka Barani Afrika wamekuwa wakiwavutia watu mashughuli, na makampuni makubwa kutoka nje kufanya nao kazi na kununua bidhaa zao kutokana na ubunifu wao kwa mfano Sarah Diouf kutoka Senegal amekuwa akijipatia wateja mashughuli kutoka nje ya Afrika.

Huduma ya afya

Kama ilivyoelezwa hapo juu fursa hutokana na matatizo au ukosekanaji wa jambo fulani. Katika upande wa afya barani Afrika matatizo yapo mengi na watu wengi wanashindwa kumuda bei za vituo vya afya na hospitali. Ikiwa hilo ni moja ya tatizo kubwa sana huduma imeanzishwa na jamii, Tanzania  ya kuwasaidia watu wasiojiweza kulipia dola 1 kwa mwezi kwa njia ya simu katika mfuko huo mdogo wa bima ya afya ili ikitokea muhusika anaumwa basi inakuwa rahisi kutibiwa.

Wajasiriamali wengine kama Ginette Karirekinyana wa Burundi na Joan Nalubega wameamua kuchukua fursa ya kutengeneza dawa za mbu za asilia, sabuni, n.k ambazo wana uhakika watu watavutiwa kuzinunua na kuzitumia ili kulinda afya zao.

Huduma za fedha za kidijitali

Inaelezwa kuwa zaidi ya 60% ya watu wazima Afrika hawatumii huduma ya benki na watu milioni 350 wanatumia simu. Hivyo baadhi ya makampuni yakatumia fursa hiyo kuwafikia wateja wao kwa kutumia simu ambazo wanakuwa nazo muda mwingi. Kwa mfano katika miezi kadhaa iliyopita Kenya kupitia kampuni za Branch na Tala imetengeneza dola milioni 135. Kwa upande wa Nigeria, kampuni nne za Cellulant, Paga, Paystack na Lidya zimezalisha takribani dola milioni 72.4.

Muziki

Tasnia ya muziki inaendelea kukua kwa kasi zaidi. Dunia nzima wanafurahia wanamuziki wa Afrika na wengi wanaendelea kujipatia majina makubwa, kutajirika na kukuza mziki huku wakiwasaidia wanamuziki wengi ambao ndo wanaanza. Watu kama Diamond Platnumz kutoka Tanzania wanaendelea kunufaika na muziki na kujitangaza ndani na nje ya Afrika, Vanessa Mdee pia anaendelea kufanya vizuri katika muziki.

Vile vile PwC imetabiri kuwa kati ya 2017 na 2021, Nigeria itakua kwa kasi katika masoko ya burudani na vyombo vya habari huku mauzo ya muziki yakifika dola milioni 88 mwaka huu.

Hivyo basi, ni vyema zaidi kama waafrika wataendelea kujituma ikiwa ni pamoja na kuunga mkono vitu vinavyotengenezwa hapa kwa sababu kama sisi wenyewe tukivutiwa navyo basi watu wa nje wataona umuhimu wa kutumia au kununua bidhaa zetu zaidi kuliko kuchukua malighafi zetu na kuzirudisha kama bidhaa kwa bei ghali.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter