Home BENKI CRDB yazindua Simu Account

CRDB yazindua Simu Account

0 comment 128 views
Na Mwandishi wetu

Benki ya CRDB leo imezindua huduma ya Simu Account ambayo itarahisisha huduma za benki hiyo kwa watumiaji. Akizindua huduma hii jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dk.Charles Kimei amesema huduma hiyo inalenga wananchi wote.

Huduma hiyo ni mfumo wa huduma za kielektroniki kutoka benki hiyo ambayo itamuwezesha mtanzania kufungua akaunti katika benki hiyo kwa kupitia simu yake ya mkononi.

Dk. Kimei ameongeza kuwa kuongeza tija katika huduma za kibenki itasaidia huduma hiyo kuwafikia watanzania wengi zaidi kwani katika watanzania milioni 50, asilimia 17 pekee ndiyo wanatumia huduma rasmi za kibenki, hali inayoashiria huduma hizi bado ni changamoto. Ameongeza kuwa huduma hii itakuwa fursa nzuri ya kuwakutanisha wanawake katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi.

Tags:

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter