Home LifestyleHealth & Fitness Benki ya Stanbic yatoa msaada wa vifaa tiba kwa hospitali ya taifa ya Muhimbili

Benki ya Stanbic yatoa msaada wa vifaa tiba kwa hospitali ya taifa ya Muhimbili

0 comment 126 views

Katika kuchangia upatikanaji wa huduma bora kwa watoto wanaozaliwa na matatizo ya kupumua, benki ya Stanbic imetoa vifaa vya tiba kwa Hospital ya taifa ya Muhimbili wodi ya wazazi.

Mchango huo ni sehemu ya juhudi za Stanbic kuchangia sekta ya afya na elimu katika jamii. Sherehe hiyo ilihudhuriwa na wafanyakazi wa benki ya Stanbic na Hospitali ya Muhimbili wakiwemo, Mkuu wa Idara ya mikopo ya Stanbic, Daniel Mbotto na Mkuu wa jengo la wazazi block c Muhimbili, Bi. Suzan Ndambala.

Mkuu wa kitengo cha Mikopo kutoka benki ya Stanbic, Bw. Daniel Mbotto (katikati) akizungumza na mkuu wa jengo la wazazi block 2 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi Suzan Ndambala (kushoto) baada ya kukabidhi ya vifaa tiba hivi karibuni kama sehemu ya kuchangia upatikanaji wa huduma bora kwa watoto wanaozaliwa na matatizo katika mfumo wa kupumua. Benki ya Stanbic imetoa mchango huo kama sehemu ya juhudi zake za kuchangia jamii katika sekta ya afya na elimu. Wengine katika picha ni wafanyakazi wa benki na MNH.

Mkuu wa kitengo cha Mikopo wa benki ya Stanbic Bank, Bwana Daniel Mbotto akimkabidhi baadhi ya vifaa tiba kwa mkuu wa jengo la wazazi block 2 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Bi. Suzan Ndambala hivi karibuni kama sehemu ya kuchangia upatikanaji wa huduma bora kwa kwa watoto wanaozaliwa na matatizo katika mfumo wa kupumua. Benki ya Stanbic imetoa mchango huo kama sehemu ya juhudi zake za kuchangia jamii katika sekta ya afya na elimu. Wengine katika picha ni wafanyakazi wa benki na MNH.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter