Home FEDHA Jinsi ya kutumia Western Union

Jinsi ya kutumia Western Union

0 comment 415 views

Ikiwa unahitaji kutuma au kupokea fedha kutoka kwa mtu, benki sio chaguo pekee. Huduma za malipo kama Western Union zinaweza kukusaidia kukamilisha mambo ambayo hayawezekani katika benki yako, lakini kutuma fedha na Western Union pia inaweza kuwa hatari, kwa hivyo unatakiwa kuwa na uhakika na mfumo unaotaka kutumia kwa ajili ya kufanya miamala ya fedha.

Western union inasifika zaidi kwa kuwa mtandao wa kutuma na kupokea fedha. Wateja wanaweza kutuma au kupokea fedha kutoka Western union katika maduka yanayotoa huduma hii. Hapa Tanzania unaweza kwenda benki na kupata huduma ya Western Union, vile vile unaweza kupata huduma hii katika maduka ya kubadilisha fedha.

Kupitia Western Union ni rahisi kumtumia fedha mtu aliye mbali kwa haraka zaidi. Pia ni rahisi na salama kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara mtandaoni kufanya miamala ya malipo kwenda sehemu mbalimbali.

Ni muhimu kuwa na uhakika na taarifa za mtu unayemtumia fedha kwa sababu ikiwa utatumia taarifa zisizo sahihi ni rahisi kutapeliwa kwani Western Union humtaka mtu anayepokea fedha kufika moja kwa moja katika mahali wanapotoa huduma hivyo kwa kukosea taarifa mtu yoyote anaweza kupokea fedha na kutoweka kusikojulikana hivyo kuleta shida.

Kuhusu ada, huwa inategemea na kiasi na namna mhusika hufanya muamala. Mtu anaruhusiwa kutuma mpaka Dola 2,999 (sawa na takribani 7,000,000) Western Union. Hadi kufikia mwaka 2018, gharama na kasi zinategemea na jinsi mtumaji atatuma fedha, jinsi mpokeaji atazipata fedha hizo na mahali zinapotumwa. Ikiwa utamtumia mtu fedha kwenda kwenye akaunti yake ya benki basi makato yatakuwa ya kawaida, na ikiwa mpokeaji wa fedha atataka kuzitoa fedha siku hiyo hiyo basi makato yatakuwa makubwa kuliko akitoa fedha hizo siku nyingine.

Kuhusu kutuma fedha kwa njia ya mtandao pia kasi na gharama zimekuwa zikitegemeana. Kwa mfano kutuma fedha kutoka katika benki yako kwenda kwenye akaunti ya mpokeaji makato ya ada huwa madogo –muamala huu huchukua siku kadhaa kukamilika . Kuhusu kupokea fedha, ada huwa kubwa kama mpokeaji atapokea fedha moja kwa moja bila  kusubiri siku kadhaa.

Zipo njia nyingi za kutuma fedha kwa watu katika maeneo mbalimbali duniani. Pia kupitia Western Union mteja huamua kama anataka fedha zake haraka (makato makubwa) au kama hana haraka sana anaweza kusubiri ili aweze kukatwa ada ndogo.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter