Home FEDHAHISA Faida na hasara za kumiliki hisa

Faida na hasara za kumiliki hisa

0 comment 268 views

Historia inaonyesha kuwa wawekezaji wengi wa hisa hujipatia mafanikio makubwa baada ya muda kutokana na uwekezaji huo. Lakini ileweke pia kuna muda thamani ya hisa hushuka hivyo wawekezaji wanatakiwa kujua kuwa kuna hatari ya kupata hasara au faida kubwa.

Faida

katika mzunguko wa biashara, kama uchumi unakua basi watu watapata kazi na kupata kipato ambacho kitawapelekea kufanya manunuzi na malipo. Malipo yakiwa makubwa basi na mahitaji na matumizi huongezeka na kusababisha kampuni na biashara kuingiza fedha zaidi. Hivyo ikiwa umewekeza hisa katika kampuni au biashara husika na inafanya vizuri katika mzunguko wake wa biashara basin a thamani ya hisa zako hupanda na kukuletea faida zaidi.

Kuwekeza katika hisa husaidia hasa katika kipindi cha mfumuko wa bei. Hata kama thamani ya hisa inaweza kushuka lakini kitendo cha kuwa mmiliki humuwezesha mwanahisa kuendelea kumiliki hisa zake hadi pale thamani itakavyopanda na kuleta faida.

Kununua hisa ni rahisi na ni mchakato wa muda mfupi kuliko uwekezaji mwingine ambao humtaka mtu kuwa na vigezo mbalimbali na kufuata hatua nyingi ili kuweza kuwekeza. Si kila mtu anaweza kuvumilia uwekezaji wenye mlolongo mrefu kwani matumizi ya fedha ni mengi, mchakato mrefu husababisha watu kutumia fedha katika matumizi mengine.

Kuwekeza katika hisa humpa muwekezaji maamuzi ya kuwekeza muda mrefu au mudamfupi. Hivyo unaweza kununua hisa baada ya muda mfupi thamani ikipanda basi muwekezaji huweza kumuuzia mtu mwingine au anaweza kuwekeza muda mrefu ili kupata faida kubwa  zaidi ikiwa kampuni au biashara inakua kwa kasi.

Hasara

Ikiwa kampuni haifanyi vizuri unaweza kupoteza hisa zako kwa sababu hakuna faida na wawekezaji katika kampuni huanza kuuza hisa zao, hata kama utauza hisa zako bado utapata hasara.

Ikiwa kampuni imefilisika basi wenye hisa huwa watu wa mwisho kulipwa au kurudishiwa fedha zilizosalia katika kampuni husika.

Kama huna uelewa na masuala ya hisa unaweza kujikuta umewekeza katika kampuni ambayo haina maisha marefu na inayoweza kufa mbeleni. Bila kuwa na ujuzi, uwekezaji katika hisa inaweza kuwa changamoto.

Uoga au kujiamini kupita kiasi kunaweza kusababisha muwekezaji wa hisa kukosa yote. Hivyo badala ya kununua hisa ndogo kwa sababu ya uoga au kununua hisa nyingi kwa sababu ya kujiamini, ni vyema kutumia vigezo vyenye mantiki ili kufanya maamuzi sahihi. Watu wengi wamepata hasara kutokana na sababu hizo mbili.

Kushindana na wataalamu wa hisa kunaweza kusababisha upate hasara hivyo tumia muda wako vizuri kwa kujifunza zaidi ili uweze kupata mafanikip mbeleni. Wataalamu huwa wanakuwa na muda, vifaa na michakato inayoeleweka. Wewe kama muwekezaji binafsi unatakiwa kuwa na ujuzi mara mbili zaidi ili uweze kufanikiwa.

Jambo la msingi la kujua ni kwamba kuna hisa katika makampuni makubwa kama Facebook, Google, Samsung n.k na kuna hisa katika makampuni ya kati na hisa katika makampuni madogo. Sio vibaya kuwekeza hisa katika kampuni kubwa, ya kati na ndogo kwa kuwa kampuni hizi hutofautiana katika ufanisi wa kazi hivyo hata faida hutofautiana.

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter