Home Elimu TICTS yachangia mabati na saruji Shule ya Sekondari Ilele

TICTS yachangia mabati na saruji Shule ya Sekondari Ilele

0 comment 129 views

Kampuni ya upakuaji wa makontena katika bandari za Tanzania ‘TICTS’ imechangia mifuko ya saruji 1,200 na mabati 1,200 katika ujenzi wa hosteli ya wasichana katika Shule ya Sekondari ya Ilele wilayani mlele mkoani Katavi.

Hosteli hiyo inakadiriwa  kutumika na wasichana takriban 200 itakapomalizika. Aliyekabidhi mchango huo ni Donald Talawa, Mkurugenzi wa maendeleo wa kampuni ya TICTS aliyeshuhudiwa na Bi. Rachel Kasanda, Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Bw Alexius Kagunze Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Mlele na  Bw Deus Bundala, Mwenyekiti wa halmashauri ya Mlele.

Bw. Donald Talawa, Mkurugenzi wa maendeleo wa kampuni ya TICTS, akiongea na wanafunzi wa shule ya Ilela secondary baada ya kukabidhi masaada wa mifuko ya saruji 1,200 na mabati 1,200 kwa ajili ya ujenzi wa hostel ya wasichana ambayo itatoa malazi kwa takriban wasichana 200. Kulia ni Bi. Rachel Kasanda, mkuu wa wilaya ya Mlele na Bw Alexius Kagunze mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mlele. Kushoto ni Bw Deus Bundala, mwenyekiti wa halmashauri ya Mlele.

Wanafunzi, waalimu na wazazi wakiwa katika shughuli ya kukabidhi mifuko 1,200 ya saruji na mabati 1,200 kutoka kwa kampuni ya TICTS kwa ajili ya ujenzi wa hostel ya wasichana katika shule ya Ilela secondary iliyopo wilayani Mlele, mkoani Katavi. Msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni 56 ulipokelewa kwa niaba ya serikali ya wilaya na Bi Rachel Kasanda, mkuu wa wilaya ya Mlele, Bw Alexius Kagunze, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mlele na Bw Deus Bundala, mwenyekiti wa halmashauri ya Mlele.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter