Home KILIMO Magufuli apongeza kufungwa akaunti za kangomba

Magufuli apongeza kufungwa akaunti za kangomba

0 comment 63 views

Raisi wa jamhuri wa muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli ameipongeza wizara ya kilimo baada ya kufunga akaunti za walanguzi wa zao la korosho maarufu kama “kangomba” katika zoezi linaloendelea la uhakiki wa wakulima wenye mashamba mikoa ya kusini.

Rais Magufuli aliyasema hayo wakati wa utiaji saini wa mauziano ya mahindi kati ya shirika la chakula duniani (WFP) na wakala wa uhifadhi wa chakula duniani (NRFA) iliyofanyika jana ikulu jijini Dar es salaam.

Akauti hizo zipatazo 3000 zimefungwa kufuatia ukaguzi wa mashamba unaondelea katika mikoa ya kusini ili kubaini wakulima halisi wa zao la korosho na walanguzi ili kufanya malipo ya zao hilo kwa watu sahihi ili kuepuka unyonyaji kwa wakulima.

Wanunuzi hao wasio na mashamba hununua korosho kwa bei ya chini kutoka kwa wakulima halafu huziuza kwa bei ya juu ili kujipatia faida.

Hivi sasa serikali chini ya wizara ya kilimo inaendelea na mchakato wa uhakiki na malipo kwa wakulima hao ambapo zaidi ya bilioni 200 zimeshalipwa kwa wakulima waliohakikiwa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter