Kahawa ni muhimu ulimwenguni, na ni muhimu kwa watu wengi. Kahawa imekuwepo katika maisha yetu na jamii zetu katika mfumo mmoja- unga baada ya kusagwa kwa kipindi cha karne 14. Ingawa hakuna ambaye anajua asili yake halisi kuna hadithi nyingi juu ya ugunduzi wake na zote husisitiza jinsi kinywaji hicho kilivyokuwa sehemu muhimu ya utamaduni wa watu wengi.
Haya ni baadhi ya mambo ambayo labda ulikuwa hufahamu kuhusu kahawa:
- Neno ‘kahawa’ linatokana na neno la kiarabu qahwah, ambalo hapo awali lilimaanisha aina ya divai. Kuna nadharia kadhaa kati ya wataalamu wa lugha juu ya ushirika wa sasa wa neno na kahawa. Wengi wanaamini kuwa kama divai, kafeini ina athari ya sumu, lakini qahwah pia hupatikana katika neno la Kiarabu quwwa, ambalo linamaanisha nguvu /nishati, au qaha ambayo hutafsiriwa kama ‘kukosa njaa’ ambapo humaanisha kuwa kahawa ni chakula ambacho huondoa njaa. Nadharia nyingine inaeleza kwamba inatoka Kaffa, katika ufalme wa Ethiopia ya zamani ambapo hutokana na mmea wa kahawa uliopelekwa Arabia kwanza.
- Hakuna mwenye uhakika kuhusu nani aliyegundua kahawa. Kuna rekodi inaeleza kuwa mtu wa kwanza kugundua kahawa alikuwa ni mchunga mbuzi anayeitwa Kaldi huko Kaffa, Ethiopia wakati wa karne ya 9. Inaelezwa kuwa Kaldi aligundua kahawa baada ya kung’oa maharage mekundu kutoka katika mmea wa kahawa, kasha kujaribu kwa kula na kuona amepata nguvu zaidi baada ya kula maharage hayo ya kahawa. Simulizi nyingine inaeleza kuwa fumbo la Sufi la Moroko, Ghothul Akbar Nooruddin Abu al-Hasan al-Shadhili, wakati mmoja alikuwa akisafiri kwenda Ethiopia na aliona ndege wanaofanya kazi kwa njia isiyo ya kawaida. Akagundua kuwa wote walikuwa wakila maharage maalum, alijaribu machache mwenyewe na akapata nguvu haraka.
- Watu hawakutumia kahawa kama kinywaji kwa muda mrefu. Baada ya kahawa kugunduliwa huko Ethiopia katikati ya 800 AD watu waliendelea kutumia kahawa kwa kuitafuna kama matunda. Hadi ilipofika karne ya 15 ambapo watu kutoka Yemen waliamua kuchemsha maharage ya kahawa na kupata kinywaji kutokana na maharage hayo.
- Katika karne ya 15 watawa wa Sufi walikunywa kahawa ili kuboresha umakini wao, sala na kukaa macho usiku kucha katika ibada.
- Kwa muda mrefu, kahawa ilikuwa ikitumika katika ulimwengu wa kiislamu. Kwa zaidi ya miaka 100, wakulima wa Yemen walipanda maharage ya kahawa na kuyatumia. Ilipofikia karne ya 16 utamaduni huo ulisambaa katika sehemu zingine za Arabia na Uturuki. Ilikuwa ikitumika katika muktadha wa kidini.
- Kahawa ilikuwa ni njia muhimu ya kuwasiliana katika jamii. Katika karne ya 16 sehemu ya kwanza ya kahawa ilifunguliwa huko Cairo, Misri karibu na chuo kikuu muhimu cha kidini baada ya hapo sehemu za kahawa zikaanza kufunguliwa hata katika mikoa mingine. Watu walipendelea kutembelea kumbi hizo na kunywa kahawa, kusikiliza muziki na kuzungumza juu ya mambo ya dini.
- Kuna kipindi kahawa ilizuiliwa huko Mecca na wasomi wa kidini mwaka 1511. Lakini marufuku hiyo ilipinduliwa na mtawala Ottoman mnamo mwaka 1524.
- Pia kanisa la Orthodox la Ethiopia lilizuia kinywaji hicho kwa sababu kilikuwa kinajulikana kama ‘kinywaji cha waislamu’. Ethiopia ilianza tena kutumia kinywaji hicho karne ya 19.
- Kahawa ilifika kwa mara ya kwanza Ulaya katika karne ya 16 kupitia watumwa wa kiislamu wa Uturuki. Ukumbi wa kahawa ulifunguliwa bara ya Ulaya kwa mara ya kwanza huko Venice mwaka 1645.