Home FEDHA Unatamani kusafiri kwa bei chee? Soma hii

Unatamani kusafiri kwa bei chee? Soma hii

0 comment 108 views

Sababu kubwa inayofanya wengi wasipende kusafiri ni gharama. Watu wengi hawaamini kama inawezekana kusafiri kwa bei nafuu.

Kama fedha ni kikwazo chako kikubwa cha kwenda kutembelea sehemu mpya, muda wa kutembelea sehemu hizo umefika. Hakikisha unazingatia mambo haya:

Usikae maeneo ya  utalii: Katika miji mikubwa, mara nyingi maeneo ya utalii huwa ni gharama kubwa hivyo hata vyumba vya kufikia, migahawa na vivutio vinavyozunguka maeneo hayo huwa na gharama. Fanya utafiti kwanza wa maeneo ya  watu wa kawaida ili kujua kama unaweza kupata sehemu ya bei nafuu. Siku hizi ni rahisi kupata sehemu ya kukaa katika miji mikubwa kupitia Airbnb hivyo unaweza kuitumia na kubana matumizi.

Weka miadi mapema: Hii ni nzuri katika upande wa tiketi. Mara nyingi tiketi za ndege zikikatwa mapema huwa  ni bei rahisi kuliko zikikatwa muda wa kusafiri. Kama una mpango wa kutembelea sehemu ambayo itakubidi kutumia usafiri wa ndege unaweza kukata tiketi yako miezi mitatu hadi sita kabla ya safari yako.

Chakula: Baada ya kula katika migahawa yenye bei unaweza kujipatia chakula katika maeneo ya watu wa kawaida kwa sababu mara nyingi wenyeji huuziwa kwa bei nafuu zaidi. Pia kwa kufanya hivyo unapata fursa ya kujaribu vyakula vipya na kujifunza utamaduni wa aina mbalimbali.

Usikope: Shida kubwa inayowakabili watu wengi ni mikopo. Kuna sababu ambazo hata ukikopa huwa zinaleta mantiki lakini kukopa kwa sababu ya kusafiri si jambo sahihi. Badala yake ni vyema kujipanga kwa kuweka akiba maalum kwa ajili ya safari yako.

Sio lazima uone kila kitu: Ni dhahiri kuwa mtu akienda sehemu mpya lazima atataka kuona na kupata uzoefu wa kila kitu lakini kadri unavyotaka kupata uzoefu na gharama nazo huongezeka. Hivyo kuepuka kutumia fedha nyingi nje ya uwezo wako, itahidi kuorodhesha mambo kadhaa ambayo ungependelea kuona katika safari yako.

Kodi chumba kinachoendana na matumizi yako: Hakuna mtu ambaye husafiri ili kuona jinsi vyumba vilivyo vikubwa katika pande nyingine ya dunia, hivyo hakuna sababu ya kukodi chumba kikubwa wakati huna matumizi nacho.

Unachotakiwa kujua ni kwamba, unaweza kuzingatia bajeti yako na kufurahia safari yako. Usitumie fedha nyingi katika hili kwa kuwa kuna mbinu mbalimbali za kufurahia safari yako ukiwa na bajeti ndogo.

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter