Home Elimu Nissan yapeleka furaha shule ya Viziwi Buguruni

Nissan yapeleka furaha shule ya Viziwi Buguruni

0 comment 164 views

KAMPUNI ya magari ya AMC Tanzania imepeleka furaha shule ya Viziwi Buguruni baada ya kukabidhi uongozi wa shule bidhaa mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi 237 wanasoma katika shule hiyo.

Kampuni ya AMC Tanzania ndio wauzaji pekee wa magari aina ya Nissan nchini.

Akikabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya AMC Tanzania, Christophe Henning  amesema kwamba wamejisikia fahari kusaidia wenye mahitaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya magari ya AMC (Nissan) Tanzania, Bw. Christophe Henning akisalimiana na wanafunzi pamoja na walimu (hawapo pichani) wa shule ya Viziwi Buguruni wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa mabegi na kompasi iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam.

Aidha alisema kwamba kampuni yake itakaa katika meza tena na uongozi wa shule hiyo kuona namna ya kuisaidia shule hiyo.

Kampuni ya AMC TANZANIA ambayo kwa sasa inatimiza miaka mitano tangu kufunguliwa nchini imesema kwamba inafanya hisani hiyo kurejesha faida kwa wananchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya magari ya AMC (Nissan) Tanzania, Bw. Christophe Henning na msafara wake wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Viziwi Buguruni wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa mabegi na kompasi iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam.

“Kama sehemu ya wajibu wetu wa kurejesha faida kwa wananchi tumeona tujikite kusaidia wenye mahitaji hasa watoto ili waweze kupata elimu katika maizngira bora kwani tunaamini viwili (watoto na elimu) hivyo ni muhimu katika maendeleo ya nchi.” alisema Henning.

Kampuni hiyo miongoni mwa bidhaa walizowapa wanafunzi ni mabegi na kompasi.

Alisema kwamba kampuni ya Nissan ambayo inatengeneza  mitambo mbalimbali inajivunia kauli mbiu yake ya ubunifu unaofurahishwa ambao umewafanya kuwa moja ya makampuni ya kutumainiwa duniani na yanayofanya biashara vyema.

Wanafunzi wa shule ya Viziwi Buguruni wakipata chakula cha mchana kilichoandaliwa na Kampuni ya magari ya AMC (Nissan) Tanzania wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa mabegi na kompasi fupi iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam

Alisema kutokana na bishara zake wanapata nafasi ya kurejesha faida kwa jamii kwa kuwekeza zaidi kwa watoto wenye mahitaji na elimu yao.

Nissan ambao kwa sasa wapo Plot No. 6, Vingunguti Area, Nyerere Road na kuwa na matawi katika miji mikuu ya kibiashara nchini kama Arusha, Dodoma, Zanzibar, Mwanza, Mbeya na Morogoro.

Katika hotuba yake mtendaji huyo aliahidi Nissan Tanzania kuendeleza ushirikiano na shule ya Buguruni kwa manufaa ya pande zote mbili ili kuleta ustawi katika jamii.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Kulwa Milembe akishukuru kwa zawadi hizo alisema kwamba wanafunzi wake wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo vifaa vya kubebea vitu wanafunzi ambao wengine wametoka nje ya Dar es salaam na familia zao ni duni sana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya magari ya AMC (Nissan) Tanzania, Bw. Christophe Henning na msafara wake wakiwa kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa shule ya Viziwi Buguruni pamoja na walimu wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa mabegi na kompasi iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam.

Alisema wanafunzi wengi wamekuwa hawana vibebeo vya madaftari, kwa hiyo msaada wa mabegi ni tunu kubwa kwao.

Alisema pamoja na msaada huo atapenda kampuni hiyo kuendelea kusaidia wanafunzi wake ili waweze kusonga mbele katika elimu.

Shule hiyo yenye wavulana 110 na wasichana 127 na kufanya jumla yao kuwa 237 ina vitengo vya msingi, ufundi, awali na wasioona.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter