Home Elimu Kusoma nje kuna faida zake

Kusoma nje kuna faida zake

0 comment 126 views

Ni fursa ya aina yake kupata nafasi ya kwenda nje ya nchi kwa ajili ya masomo. Japokuwa kuna vyuo vyenye hadhi ya kimataifa hapa nyumbani na elimu inayotolewa ina ubora wa hali ya juu, bado kusoma nje ya Tanzania kuna faida lukuki.

Ikiwa umepata nafasi ya kwenda kusoma nchi nyingine, fanya hivyo mara moja bila kusita kwani kusoma nje kuna faida mbalimbali.

Hapo chini ni baadhi ya faida za kusoma nje ya Tanzania.

-Lugha

Unaposoma nje ya nchi, mara nyingi inakulazimu kujifunza lugha ya nchi husika. Hii inaweza kukusaidia hata baada ya kumaliza masomo yako kwa kuwa unakuwa na kitu cha ziada pale wakati wa kutafuta kazi unapofika. Watanzania wengi wanaosoma China hulazimika kujifunza kichina na uwezo wao wa kutafsiri lugha hiyo imesaidia baadhi yao kuajiriwa.

-Elimu

Inawezekana kwamba mfumo wa elimu uliopo nchini Tanzania ni tofauti na ilivyo katika mataifa mingine. Kwa kusoma nje ya nchi, unapata fursa ya kujifunza mfumo wa tofauti na nyumbani hivyo kupata maarifa ya ziada na kuongeza ujuzi.

-Ajira

Baadhi ya makampuni hupendelea kuajiri watu waliosoma nje ya nchi kwa kuwa wanaamini kwamba elimu waliyopata ni bora zaidi. Makampuni ya kigeni au ofisi za balozi mbalimbali hapa nchini ni mfano mzuri, kwani asilimia kubwa huajiri zaidi wale waliosoma nje ya nchi. Ni nadra sana kwa watu waliosoma nje na kupata matokeo mazuri kukosa ajira.

-Utamaduni

Unapotembea mbali na nyumbani, unapata nafasi ya kujua namna watu wengine duniani wanavyoishi na kujifunza utamaduni wao.

-Marafiki na mahusiano ya muda mrefu

Hii ni fursa nzuri ya kutengeneza marafiki wa kudumu kutoka nchi mbalimbali. Hata baada ya hapo, unapotaka kwenda nchi nyingine na tayari unafahamiana na mtu kutoka huko, inakuwa rahisi kupata muelekeo, tena kutoka kwa mtu ambaye tayari unamfahamu. Pia hii husaidia kujua sehemu nyingine kwa undani zaidi.

-Uzoefu

Ikiwa unasoma nje ya nchi, mbali na mazingira ambayo umezoea, unapata uzoefu zaidi kutokana na hali ya maisha ya sehemu ulipo. Unaweza kupata wazo jipya la biashara ambali labda hujawahi kuona au kufikiria na kulitekeleza mara baada ya kurudi nchini.

-Utalii

Mbali na kupata elimu, unapoenda kusoma nchi nyingine, unapata nafasi ya kuwa mtalii na kutembelea maeneo mbalimbali na kufahamu ulimwengu zaidi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter