Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Nukuu (Quotes) 25 za Mo Dewji

Nukuu (Quotes) 25 za Mo Dewji

0 comment 397 views

Mohammed ‘Mo’ Gulamabbas Dewji (44) ni bilionea kijana zaidi barani Afrika na kwa mujibu wa jarida maarufu la Forbes, utajiri wake unakadiriwa kuwa ni takribani Dola 1.9 bilioni za Marekani hadi hivi sasa.

Mara kwa mara, Mo amekuwa akitumia ukurasa wake wa Twitter kuhamasisha, kuelimisha na kushawishi vijana wajasiriamali kuendelea kupigania ndoto zao na kutokata tamaa.

Hizi ni baadhi ya Nukuu (Quotes) zake maarufu:

  1. Anayejitahidi atafaidi.
  2. Huwezi kujua unachoweza mpaka ujaribu.
  3. Kamwe wewe sio mzee sana kujifunza.
  4. Aliye na hamu ya kupanda juu hukesha.
  5. Hakuna kitu kinaua urafiki kama mikopo.
  6. Aliyetangulia katangulia, anayefuata akazane.
  7. Hutaona matokeo ikiwa hufanyi unachofanya mara kwa mara.
  8. Kinachokuja kirahisi, hakiwezi kudumu. Kinachodumu, hakiji kirahisi.
  9. Tumia vizuri kila muda unaopata kufanya kitu chenye faida kwenye maisha.
  10. Acha kujilinganisha na watu wengine. Mtu pekee wa kushindana naye ni wewe mwenyewe.
  11. Wakati wa kuwekeza katika maendeleo ya Afrika ni sasa. Inabidi tutumie vizuri kila fursa iliyopo mbele yetu ili tufanikiwe.
  12. Mungu hatupatii mtihani tusioweza kukabiliana nao. Kuwa na subira. Kila kinachotusibu kitadhihirisha kuwa kitu tutakachoweza kukishinda.
  13. Muda ni kila kitu. Kwa mipango ya Mungu, kumbuka hamna kinachowahi wala kuchelewa. Kilicho na maana kwako kitakufikia.
  14. Safari ya mtu mwingine haiwezi kukuzuia wewe kufanikiwa kwenye safari yako. Usipoteze muda kwenye mawazo yasiyokuwa na umuhimu.
  15. Wekeza muda wako katika mambo yatakayokusaidia kukua na kujiendeleza. Maisha ni mafupi mno kushiriki katika mazungumzo yasiyokuwa na maana.
  16. Usiogope changamoto za maisha, muogope Mungu peke yake. Yeye ndiye mwenye kutoa riziki kwa kila mtu.
  17. Kuwa na nidhamu sana, mvumilivu sana. Kuwa na maadili sana na ufanye kazi kwa juhudi. Kwa mapenzi ya Mungu mafanikio yatakuja.
  18. Kosa kubwa ambalo naona watu wanafanya leo ni kutaka mafanikio ya haraka, pesa za haraka na umaarufu wa haraka. Sio sahihi na haiwezi kukufanya kuwa na furaha. Huwezi kuzingatia kama una haraka!
  19. Mustakabali wa maisha yako ya baadaye haujitengenezi au kuandaliwa kwa hali uliyonayo sasa. Ili ufanikiwe, unapaswa kuwa makini na thabiti. Uthubutu wako ndio ufunguo wa mafanikio yako.
  20. Kuweza kukabiliana na kushindwa, kudhibiti hatari mara kwa mara na kufaulu baada ya mashaka ndiyo kinachofanya mtu awe mjasiriamali bora.
  21. Changamoto ni sawa na mpinzani wako na mpinzani wako atakuwa mpinzani wako iwapo tu utamruhusu.
  22. Ni muhimu kufahamu kuwa mafanikio sio lazima kuwa yanapatikana ughaibuni tu. Kuna nafasi hapa nyumbani ambazo ukizifanyia kazi unaweza ukafanikiwa.
  23. Kwanini watu huuliza kama una kazi nzuri, una gari zuri, umeoa/ umeolewa, unamiliki nyumba? Maisha sio orodha ya vitu. Haijalishi ikiwa mtu ana chochote katika vilivyooredheshwa hapo juu. Wote tuna mwisho na niamini ninachokuambia, sio gari wala nyumba itakufikisha huko.
  24. Huwezi kukua kama hutengi muda kuongeza nguvu. Kumbuka, kama mfano wa gari, tunahitaji matunzo na kuongezwa mafuta. Na hilo haliwezi kufanyika ikiwa gari daima linaenda. Usidharau uwezo wa likizo ya siku moja.
  25. Vitu vingi katika maisha vinaweza kujaribu kukuondoa kwenye malengo yako lakini usipoteze muelekeo. Mipango inaweza kubadilika lakini kamwe sio mwisho wa safari.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter