Home AJIRA Biteko kuongoza wizara ya madini

Biteko kuongoza wizara ya madini

0 comment 220 views

Rais John Magufuli amemteua Mh.Doto Biteko Mashaka kuwa waziri kamili wa madini akichukua nafasi iliyokuwa ikimilikiwa na Mh.Angela Kairuki aliyehamishwa na kuwa waziri wa nchi,Ofisi ya waziri mkuu,atakayeshughulika na uwekezaji.

Akitangaza mabadiliko hayo,Katibu mkuu kiongozi,John Kijazi amebainisha pia kuhusu teuzi zingine za makatibu wakuu,manaibu katibu wakuu,balozi na Katibu Tawala ambao wataapishwa hapo baadaye.

Kabla ya uteuzi huo,Biteko alikua naibu waziri wa madini akisaidiana na Stanslaus Nyongo ambaye ataendelea kuwa naibu waziri katika wizara hiyohiyo akimsaidia Biteko.

Biteko Mwenye taaluma ya ualimu amepitia ngazi mbalimbali za uongozi tangu akiwa mwanafunzi ambapo alikua ni Rais wa serikali ya wanafunzi chuoni katika chuo cha mtakatifu augustino cha jijini mwanza na baadaye alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la bukombe akimshinda profesa Kahigi aliyekua mwalimu wake wa chuo kikuu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter