Home AJIRA Mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu pesa

Mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu pesa

0 comment 261 views

Ili ufanikiwe katika maisha ni lazima uwe na nidhamu ya pesa.Kua na nidhamu ya pesa ina maanisha kua na matumizi yenye mpangilio na faida kwako ama biashara yako,ili kufanikisha hilo basi zingatia haya,

 

  • Usikope pesa ya riba ili uanzishe biashara.

Ukiwa unataka kuanza biashara ya aina yoyote ile epuka kukopa pesa itakayokulazimu uirudishe na riba. Kukopa pesa kwa riba kutafanya biashara yako kukua taratibu sana maana inawezekana badala ya kupata faida wewe unakua unalipa riba ya mkopo uliochukua ili kuanza biashara.

 

  • Usiingie matumizi ya pesa ambayo haipo katika mikono yako.

Kuingia matumizi au kufanya matumizi au kumuahidi mtu pesa uliyoahidiwa mahala fulani ni kosa kubwa. Mfano kukopa bidhaa dukani kwa ahadi ya kulipa pesa unayotegemea kuipata kutoka kwa mtu mwingine,hivyo basi ni bora kufanya matumizi yako kwa pesa iliyo katika uwezo wako na kwa kipindi kilichopo.

 

  • Zingatia matumizi ya pesa.

Kama unataka kutunza ama kuhifadhi pesa,weka pembeni kiasi unachodhani unatakiwa kutunza kwanza alafu fanya matumizi yako kwa kiasi kitakachokua kimebaki,epuka kila unapopata/pokea pesa,kufanya matumizi kwanza alafu pesa itakayokua imebaki ndio ukaifanya kua akiba. Kufanya hivi kutafanya wewe usiwe na matumizi yasiyo ya lazima.

 

  • Omba mawazo sio pesa.

Kuna msemo usemao ukutanapo na mvuvi usiombe samaki,omba ndoano ili ukavue samaki mwenyewe.Vivyo hivyo katika maisha ya biashara iwapo utakutana na mtu ambae ni tajiri ama anajiweza kiuchumi,unashauriwa usimwombe pesa bali jaribu kuongea nae akupe njia za kupata pesa,sio kukupatia pesa.

 

  • Kua na nidhamu ya pesa.

Maana halisi ya kua na nidhamu ya pesa ni kuheshimu matumizi ya pesa,ikimaanisha kua ni lazima kuwe na mipangilio sahihi ya matumizi pia kujua pesa kiasi gani itumike katika biashara zako ili ziweze kuendelea kukua na kiasi gani kitumike katika matumizi yasiyo kua na athari zozote katika biashara yako.

 

Hayo ni baadhi ya mambo muhimu ya kuzingatia katika utunzaji na matumizi ya pesa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter