Home AJIRA Njia 3 za kuchochea ubunifu

Njia 3 za kuchochea ubunifu

0 comment 136 views

Kutengeneza kitu kutoka kwenye wazo sio kazi rahisi. Hamasa, jitihada na muelekeo ni silaha sahihi kufanikisha hili japokuwa mara nyingi sio rahisi kuwa na vitu vyote vitatu kwa wakati mmoja.

Hbari nzuri ni kwamba, kuna mbinu ambazo tunaweza kutumia ila kuhakikisha kuwa hatubaki nyuma na tunaendelea kuwa wabunifu katika biashara na kazi zetu za kila siku. Hapo chini ni njia tatu unazoweza kutumia kuchochea ubunifu katika maisha yako.

1. Usibaki nyuma

Huwezi kujua uwezo wako kama unafanya kitu hicho hicho kila siku. Kukaa kwenye dawati lako ofisini hakutakufanya uwe mbunifu na kufikiria mbali. Badala yake, toka nje, jifunze na jionee kwa macho. Tunatumia muda mwingi sana kukaa mbele ya kompyuta zetu na hivyo tunakandamiza uwezo wetu wa kufikiria mbali. Tafiti mbalimbali zilizofanywa zimegundua kuwa kutoka nje ya ofisi na kutembea huchochea ufikiri pamoja na uwezo na kutatua changamoto zinazotuzunguka. Wakati mwingine unahitaji kupumzika na kuruhusu akili yako kupata mwanya wa kufikiri.

2. Jifunze vitu vipya

Watu wengi hupenda kufanya vitu kwa mazoea. Lakini kama unafanya kitu kimoja kila siku, ni nadra sana kuwa mbunifu na kupata mawazo makubwa. Ni muhimu kutenga muda na kukutana na watu wapya, kwenda sehemu tofauti na kujifunza masuala mbalimbali kutoka kwa watu wengine ili kuweza kufikiria vitu vipya na kuwa na mawazo tofauti.

3. Epuka vishawishi, fanya kazi

Muda wa kazi unapofika ni vizuri kuweka vitu vyote ambavyo vitakufanya upuuzie kazi. Vitu kama simu vinaweza kukurudisha nyuma hivyo unaweza kuweka pembeni simu yako na kutimiza majukumu yako yote bila usumbufu wowote. Wabunifu wengi hutenga muda maalum kwa kazi tu na hivyo wanapata muda wa kutosha wa kufanya kazi kwa umakini wa hali ya juu.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter