Home BIASHARA Bandari kavu kujengwa Mbeya

Bandari kavu kujengwa Mbeya

0 comment 128 views
Na Mwandishi wetu

Uongozi wa mkoani Mbeya unafanya mpango wa kujenga bandari ya nchi kavu na kituo cha biashara kwa ajili ya kukuza uwekezaji nchini. Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amosi Makalla amesema kuwa serikali imejipanga vema kubadilisha mkoa huo na kuimarisha shughuli zinazochangia uchumi.

Baada ya kufanya ukaguzi katika eneo lililotengwa na halmashauri ya Mbeya kwa ajili ya ujenzi huo, Makalla amesema sekta za viwanda na kilimo zitanufaika sana na ujenzi huu ambao baada ya kukamilika utasaidia wafanyabiashara hasa wa nchi za kusini, ambao kwa sasa inabidi wasafiri hadi Dar es salaam kwa ajili ya kuchukua mizigo

Makalla pia amewaomba wananchi mkoani Mbeya kutumia fursa kama hizi za kiuchumi na pia kuutunza mkoa huo badala ya kujihusisha vya vitendo visivyo na tija wala manufaa kwa mendeleo yao.

Wafanyabiashara mkoani humo nao wameshauriwa kutumia nafasi hii kuingizia biashara ambazo zitakidhi ushindani kwenye soko la kimataifa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter