Home BENKI Benki zatakiwa kupunguza riba

Benki zatakiwa kupunguza riba

0 comment 135 views

Benki mbalimbali nchini zimetakiwa kupunguza riba, ili kutoa fursa kwa wateja kukopa na kufanya uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa ametoa rai hiyo jijini Arusha katika mkutano wa wadau wa Benki ya Maendeleo (TIB), Kanda ya Arusha.

Mtahengerwa amesisitiza kuwa endapo benki zikipunguza riba katika mikopo, Watanzania wengi wataweza kukopa na kufanya uwekezaji wenye tija utakaoinua uchumi wa nchi, badala ya wawekezaji wa nje kuja nchini kuwekeza.

Amesema “benki punguzeni riba ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara kuwekeza zaidi nchini badala ya kutegemea wawekezaji kutoka nje ya nchi pekee waje kuwekeza nchini, tunataka Watanzania wawekeze kupitia benki na kuwa mamilionea kutoka  nchini.”

Naye Kaimu Mkurugenzi wa TIB, Lilian Mbassy amesema katika kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma, benki hiyo imekutana na wateja wao kutokana na kutambua umuhimu wa sekta binafsi katika shughuli za kiuchumi nchini.

Aidha amesema katika kuadhimisha wiki hiyo,benki hiyo pia imechagua kufanya kazi za jamii ambapo wamefanya usafi katika kituo cha daladala simu 2000 kilichopo manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter