Home BENKI Jinsi ya kuwa salama mtandaoni

Jinsi ya kuwa salama mtandaoni

0 comment 181 views

Uwezo wa kutumia huduma ya benki kwa kupitia mtandao umeleta urahisi zaidi katika maisha ya watu wengi lakini pia imekuwa ni fursa kwa wezi. Inaelezwa kuwa kutumia huduma ya benki kwa kutumia mtandao ni salama zaidi ikiwa ni pamoja na kutokurahisisha wezi kupora fedha zako.

Lakini kuna baadhi ya vitu ambavyo unaweza kufanya ambavyo vinaweza kusababisha fedha zako zisiwe salama, hivyo zingatia haya kuhakikisha unafanya miamala ya benki kwa usalama kupitia mtandao:

Taarifa binafsi.Watu wengi wametapeliwa kwa sababu ya kutoa habari binafsi wakidhani kuwa ni benki zao ndio zinahitaji habari hizo. Hivyo kuwa makini, usitoe habari zako binafsi kuhusu akaunti yako kwa mtu yeyote ambaye atakuuliza kwani hata siku moja, benki yako haiwezi kuuliza habari zako ikiwa ni pamoja na namba yako ya simu, barua pepe, akaunti namba au hata neno la siri. Ndio maana hata Polisi imekuwa ikijitahidi kuwakumbusha wananchi kuhusu suala la wizi unafanywa mtandao na watu wanaotuma ujumbe wakimtaka mhusika kutuma fedha katika namba ngeni au wengine wanaopiga simu na kudai kuwa wanahitaji taarifa za mhusika ili wamtumie kiasi cha fedha. Ni muhimu kuwa makini na kuhakikisha kuwa taarifa zako binafsi unazijua mwenyewe.

Watu wanatakiwa kuwa makini na mitandao ya umma ikiwa ni pamoja na maunganisho ya data katika migahawa, maduka, hoteli n.k hasa wakiwa wanataka kufanya miamala ya fedha kupitia mtandao kwa sababu huwa hakuna usalama wa kuaminika. Ikiwa ni muhimu kufanya muamala muda huo basi tumia data ya simu yako ya mkononi .

Vilevile  ni muhimu kutumia programu za kisasa na vifaa vya kisasa ukiwa unafanya miamala kupitia mtandao hii itakusaidia kuepukana na vitisho au usumbufu usio na muhimu. Epuka kutumia kompyuta za zamani au ambazo hazijaidhinishwa kufanya miamala ya kifedha.

Ikiwa akaunti yako itakuwa imeathiriwa na udanganyifu au makosa basi itakuwa rahisi kulindwa (katika akaunti yako binafsi). Unashauriwa kutoa taarifa katika benki yako husika ili kuhakikisha tatizo lolote linapewa usumbufu kwa haraka na ulinzi unaendelea kuwa wa juu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter