• Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
Tuesday, June 28, 2022
  • Login
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
No Result
View All Result

MPANGO MPYA WA UTALII KUZINDULIWA DAR JULAI MOSI

Mpango mpya wa kukuza utalii wa ndani unatarajiwa kuzinduliwa Julai 1,mwaka huu jijini Dar es salaam.

Jensen Kato by Jensen Kato
June 30, 2020
in BIASHARA, UWEKEZAJI
0
Share on FacebookShare on Twitter

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla anatarajiwa  kuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa mkakati huo sambamba na viongozi wengine waandamizi kutoka serikali na pamoja na wadau wa utalii hapa nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari jijini Dares Salaam mapema hii leo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mpango huo Bw Mkumbwa Ally alisema mpango huo unaojulikana kama Domestic Tourism Promotion Initiative (DTPI) unalenga kutangaza utalii wa ndani kwa watanzania pamoja na raia wa kigeni kuhusu vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini.

“Ni mpango unaohusisha juhudi mahsusi katika kusaidiana na  serikali  kukuza utalii wa ndani na kupunguza athari za janga la Corona kwenye sekta hii muhimu.’’ Alibainisha Bw Mkumbwa.

Mkakati huo wenye kauli mbiu ‘Utalii Mpya.Fursa Mpya’ unaratibiwa kwa pamoja  baina ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT) na  kampuni ya Real PR Solutions ya jijini Dar es Salaam.

Alisema hafla hiyo fupi itahusisha pia ushiriki wa viongozi waandamizi wa serikali na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii wakiwemo Bodi ya Utalii  Tanzania (TTB), Chama cha Mawakala wa Utalii Tanzania (TATO), Chama cha watoa huduma za utalii wa ndani  (TLTO) na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).

Wengine ni pamoja na Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania (TFS),Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro, Taasisi ya Sekta binafsi, Chama cha wamiliki wa hoteli pamoja na wadau wengine.

ADVERTISEMENT

“Zaidi pia tumewaalika Waziri  wa Viwanda na Biashara , Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Waziri wa Afya  kutokana na michango yao katika ustawi wa sekta ya utalii hapa nchini .” Alisema.

Alitaja baadhi ya mambo muhimu kwenye kampeni hiyo ambayo yatatekelezwa kwa awamu kuwa ni pamoja na Mafunzo kwa vijana kote nchini ili waweze kunufaika na mnyororo wa thamani katika sekta ya utalii ikiwemo kuongoza watalii, mafunzo ya huduma kwa wateja katika hoteli na migahawa, vyombo vya usafiri na ujuzi wa kufungua kampuni za utalii.

“Tunatarajia mafunzo haya yatawanuisha vijana zaidi 100,000 hususani wale wasio na ajira ili waweze kutambua fursa zilizopo kwenye sekta ya utalii na wazitumie vizuri.’’ Alisema Mkumbwa ,.huku akiitaja mikoa itakayoanza kunufaika na mpango huo kuwa ni pamoja na mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mwanza, Geita, Kagera, Simiyu, Mara na Shinyanga.

Alisema katika kuupamba mkakati huo kutakuwa na uhusishwaji wa matukio mbalimbali ya kimichezo na burudani ili kuvutia walengwa zaidi wa mpango huo.

“Mkakakati huu unahusisha matukio mbalimbali yanayolenga kusaidia ukuaji wa sekta ya utalii nchini na kukuza  uchumi wa ndani, lakini pia kuisaidia serikali na wafanyabiashara kuamsha tena biashara zilizokuwa zimezorota kufuatia janga hili la Corona na hatimaye tukuze uchumi wa nchi,’’ alisema Mkumbwa.

Alisema tahadhari zote za kiafya zitachukuliwa kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona katika matukio yote yaliyomo kwenye mpango huo.

Jensen Kato

Jensen Kato

Next Post

Jinsi ya kuwa salama mtandaoni

Discussion about this post

Habari Mpya

Kilimo biashara, sekta yenye fursa za uwekezaji

June 27, 2022

Miamala ya simu yaongeza Pato la Taifa

June 24, 2022

Mapendekezo bima ya afya kwa wote

June 23, 2022

Turkish Airlines yarejesha safari zake KIA

June 22, 2022
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla akizungumza katika warsha ya viongozi wa Serikali wa mkoa na Bank ya NMB.

Benki ya NMB yapongezwa

June 22, 2022

Rais Samia azindua taasisi Zanzibar

June 20, 2022

KUHUSU SISI

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905. PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.

LATEST

Kilimo biashara, sekta yenye fursa za uwekezaji

by Jensen Kato
June 27, 2022
0

Kilimo biashara kinaendelea kukua barani Afrika na muda umefika kwa watu hususani vijana kuchagamkia fursa mbalimbali zinazotokana na kilimo. Watu...

Miamala ya simu yaongeza Pato la Taifa

by Pesatu Reporter
June 24, 2022
0

Miamala ya fedha kwa njia ya simu imechangia kuongezeka kwa pato la Taifa kutoka asilimia 40 mwaka 2013 hadi kufikia...

RECOMMENDED

Waziri Mwijange aja na orodha ya viwanda visivyofanya kazi

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

  Na Mwandishi wetu. Baada ya Rais John Magufuli kuonyesha kukerwa na kitendo cha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji...

Nane Nane itumike kama darasa huru kwa wakulima

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

Na Mwandishi wetu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejitolea kuwapa mafunzo ya siku moja wakulima mkoani Lindi...

No Result
View All Result
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI

© 2022 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In