Home BENKI Maswali ya kuuliza kabla ya kufungua akaunti benki

Maswali ya kuuliza kabla ya kufungua akaunti benki

0 comment 141 views

Tekinolojia zinaendelea kuboreshwa na kukua kwa kasi sana duniani hali inayopelekea mambo mengi kurahisishwa ikiwa ni pamoja na jinsi ya kuhifadhi fedha. Licha ya maendeleo yanayoendelea kufanyika benki zimeendelea kuwa muhimu kwa watu hasa katika suala zima la usimamizi wa fedha, mikopo nk.

Hivyo ikiwa  unataka kufungua akaunti ya benki kwa mara ya kwanza, au hauridhiki na benki yako ya sasa, kupitia maswali yafuatayo utaweza kufanya chaguo sahihi la benki ambayo utakuwa unahifadhi fedha zako na kunufaika na  huduma nyingine mbalimbali kutoka katika benki husika:

Je, kuna ada ya kila mwezi? Na kama ipo unaweza kuepukana nayo vipi?

Benki nyingi huchaji ada ya kila mwezi katika akaunti zao za msingi za kuhifadhia fedha lakini kupitia vigezo mbalimbali mmiliki wa akaunti anaweza kuepukana na makato hayo. Kwamfano kuna vigezo tofauti kwa wamiliki wa kawaida, wanafunzi na muda mwingine wafanyakazi hivyo ni vyema kujua mpango mzima wa makato ya ada upoje katika benki husika kabla ya kufanya maamuzi.

Mashine ipi ya ATM unaweza kutumia bure?

Benki  nyingi huruhusu kutumia mashine zao za ATM bila malipo, lakini si kila wakati mtu ataweza kutoa fedha katika mashine ya ATM inayohusika na benki hiyo.kutumia ATM ya nje  ya mtandao wa benki yako kunaweza kukugharimu ada kutoka katika benki yako na pia kutoka kwa mmiliki wa ATM na/au mtandao hivyo ni vizuri kujua mchakato mzima kuhusu utoaji wa fedha katika mashine za ATM hasa za benki tofauti.

Je, kuna gharama za kulipa bili mtandaoni?

Benki nyingi zimewarahisishia wateja wao kufanya malipo kupitia mtandao mahali popote hivyo badala ya kwenda benki kuchukua fedha kwaajili ya kulipa bili siku hizi unaweza kufanya malipo kupitia vifaa vya kielektroniki kama simu, kompyuta nk ambapo baadhi ya benki hutoa huduma ya bure ya malipo kupitia mtandao huku benki nyingine huchaji ada baada ya mteja kufanya malipo kupitia mtandao hivyo ni muhimu kujua taratibu za benki husika.

Utapataje msaada ikiwa mambo hayatokwenda sawa?

Benki yako inaweza kuwa na matawi ya karibu ambayo unaweza kwenda kupata msaada ikiwa matatizo yatatokea. Kujua mapema jinsi benki yako itafanya kazi na wewe katika shida au matukio ambayo itakubidi wakupe usaidizi ili kuweza kusuluhisha changamoto mbalimbali kutaweza kukusaidia kufikia azimio haraka zaidi ikiwa umekumbana na changamoto yoyote, na kukufanya uwe na ujasiri zaidi katika uchaguzi wako wa benki.

Utanufaikaje kupitia benki hiyo?

Benki nyingi hutoa tuzo mbalimbali kwa wateja wao ili kuwahamasisha kuendelea kutumia huduma zao. Hivyo si vibaya kuuliza benki husika kuhusu mambo ambayo unaweza kunufaika nayo kwa kufungua akaunti katika benki hiyo.

Ni muhimu kuhakikisha unafungua akaunti katika benki ambayo itakidhi mahitaji yako ikiwa ni pamoja na usalama wa fedha zako, riba nafuu nk.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter