Home BENKI Tanzania yaridhia mtaji AfDB kuongezwa

Tanzania yaridhia mtaji AfDB kuongezwa

0 comment 117 views

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema Tanzania inaunga mkono Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kutaka kuongezewa mtaji kutoka Dola za Marekani 94.76 bilioni hadi 268.6 bilioni ikiwa ni ongezeko la takribani asilimia 200, kwa kuwa itawezesha benki hiyo kutekeleza majukumu ya utoaji mikopo kwa nchi wanachama, na hivyo kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa ujumla.

Waziri Mpango amesema hayo akiwa nchini Marekani baada ya mkutano wa saba wa magavana ambao pia ni mawaziri wa fedha kutoka nchi wanachama 54 za benki hiyo na kuongeza kuwa, AfDB imetoa mabilioni kwa Tanzania ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, ndiyo maana inakubaliana na uamuzi huo wa kutaka kuongezewa mtaji.

“Wakati umefika ili twende haraka zaidi, mitaji sehemu nyingine imepungua, pendekezo la kuongeza mtaji wa benki hii ni jema na matokeo ya miradi inayofadhiliwa na benki hii yanaonekana katika nchi zetu za kiafrika kwa sababu benki hii iko Afrika na inaijua Afrika tofauti na benki nyingine”. Ameeleza Dk. Mpango.

Miongoni mwa miradi iliyofadhiliwa na benki ya AfDB hapa nchini ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya barabara, maji, kilimo na nishati.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter