Home BIASHARA Tanzania kuuza mazao Sudan

Tanzania kuuza mazao Sudan

0 comment 130 views

Tanzania itaanza kuuza bidhaa za nafaka nchini Sudani Kusini baada ya Bodi ya Mazao Mchanganyiko Tanzania (CPB) kwenda nchi kutafuta fursa za kuuza mazao.

Mazao hayo ni pamoja na mahindi, mchele, maharage, una wa sembe na wa dona.

Bodi hiyo imesema imejipanga na ipo tayari kuanzia sasa kuuza mazao kwenye nchi hiyo kutokana na uhitaji wake.

Naibu Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Sudan Kusin, Salwa Monytuil amesema milango ipo wazi kwa wafanya biashara wa Tanzania kupeleka bidhaa mbalimbali.

Amesema “hii ni fursa kwetu na kwa Tanzania kufungua milango kwa kila mmoja na ulimwengu ili tuweze kusonga mbele.”

Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa CPB amesema Valeriana Mablangeti amesema serikali za nchi hizo mbili zimekuwa zikijadiliana kwa mda mrefu kuhusu maswala ya biashara na kama Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanapaswa kufanya kazi kwa pamoja.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter