Home BENKI BoT kuanza kununua dhahabu

BoT kuanza kununua dhahabu

0 comment 81 views

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dk. Bernard Kibesse amesema kuwa BoT haina tatizo lolote linalopelekea kushindwa kununua dhahabu kwani hadi kufikia mwaka 1994, benki hiyo imekuwa ikifanya hivyo. Dk. Kibese amesema hayo katika mkutano wa wachimbaji, wafanyabishara na wadau wa sekta ya madini jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa, BoT ipo tayari kununua dhahabu moja kwa moja kutoka kwa wachimbaji

“Tunafahamu kuwa ‘Reserve’ za Benki kuu nyingi duniani zinakuwa na hazina za dola na dhahabu, nasi tunaweza na tupo tayari kuanza kununua tena. Tunaelewa Benki kuu nyingi zinakuwa na hazina ya dhahabu”. Amesema Naibu Gavana huyo na kuongeza:

“Tuko tayari kununua dhahabu ambayo tayari iko ‘refined’ kwa sababu ndiyo kiwango ambacho kinakubalika kimataifa na nimefurahi kusikia kuwa kuna watu wana mitambo ya kufanya hivyo. Benki kuu tumeandaa sehemu ya kuhifadhi madini ndani ya utaratibu maalum ambazo tutakubaliana kuwa ni lazima dhahabu inayokuwa pale iwe na mpangilio wake wa uhifadhiwaji. Kwa mfano mnunuzi hajapatikana hiyo dhahabu hairuhusiwi kukaa hapo zaidi ya siku tano na badala yake ipelekwe Center’.”  Amesema Dk. Kibese.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter