Home BIASHARA Bei ya mafuta yaathiri soko la gesi

Bei ya mafuta yaathiri soko la gesi

0 comment 142 views

Kufuatia tamko lililotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (EWURA) kuhusu ongezeko la bei ya mafuta ikielezwa kuchangiwa na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia ambapo petrol imepanda kwa Sh.55 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 2.4, dizeli (Sh.19) sawa na asilimia 0.88 na mafuta ya taa (Sh.36) au aslimia 1.68 imechochea ongezeko la bei ya gesi ya kupikia nchini.

Hayo yamesemwa na Meneja wa maendeleo ya biashara Oryx, Mohammed Mohammed ambaye amedai kupanda kwa bei ya gesi ya kupikia nchini ni matokeo ya kupanda kwa bei ya mafuta kwa sababu ya mafuta hayo kutumika kama ghafi.

Soma Pia Walioficha mafuta ya kula, sukari waonywa

“Bei ilipanda muda mrefu lakini tulijitahidi kubaki na bei ya awali tukijipa moyo itashuka lakini baadae tuliona tunazidi kuumia” Alisema Mohammed.

Imeelezwa kuwa mara nyingi bei ya gesi imekuwa ikipanda kwa kiwango cha kuanzia Sh.1000 hadi Sh.3000 katika maeneo mbalimbali hapa nchini

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa wakala wa serikali wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja (PBPA) akielezea suala hilo amedai kuwa ni vigumu kwa mamlaka hiyo kupanga bei maalum kutokana na wasambazaji kuuza kutokana wasambazaji kununua kulingana na uhitaji, hivyo uuzaji wao umekuwa ukienda sambamba na gharama walizotumia na inapoingizwa nchini huuzwa kutokana na gharama iliyotumika katika manunuzi.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter