Home BIASHARA Biashara isikose vitu hivi

Biashara isikose vitu hivi

0 comment 101 views

Kuanzisha biashara na kuhakikisha inaendelea si jambo rahisi na ndio maana ni asilimia chache tu ya biashara zinazoanzishwa hufanikiwa. Inaelezwa kuwa kwa wastani, ni biashara 1 kati ya 10 zinazoanzishwa huendelea. Wajasiriamali hupitia vikwazo mbalimbali wakati wa kuanzisha biashara zao. Kuna sababu nyingi zinazoweza kupelekea biashara ishindikane.

Haya ni mambo 10 yanayoweza kupelekea biashara ifanikiwe:

Muelekeo

Kila biashara inayoanzishwa huhitaji kiongozi anayefikiria mbali, ili katika nyakati ngumu aweze kujua anapambana vipi na matatizo ili kuifikisha biashara pale inapotakiwa kufika. Kiongozi mzuri ni yule ambaye anazingatia malengo ya baadae huku akitoa suluhisho katika mahitaji ya haraka.

Soko

Biashara yoyote inayoanzishwa haitakiwi kuwa nyuma kuhusu suala  hili kutokana na maendeleo yaliyopo katika teknolojia. Ni muhimu kujua uharaka wa kuzalisha na kufikisha bidhaa utaleta wateja zaidi. Moja ya sababu inayopelekea biashara zifanikiwe ni uwezo wa kuwafikia wateja kwa haraka zaidi.

Fedha

Biashara nyingi zilizofanikiwa zinajua jinsi ya kufanya kazi ndani ya bajeti. Uwezo wa kusimamia fedha na kuepusha kampuni inayoanza na madeni ni moja ya vitu vinayoweza kusababisha kampuni ifanikiwe. Ni muhimu kwa kampuni inayoanza kufanya kazi zaidi na kutumia fedha kidogo.

Mtandao

Kama ilivyo katika masuala mengine, kuwa na mtandao na kufahamiana na watu wa aina mbalimbali huipeleka mbali kampuni. Kwa mfano kutumia mitandao ya kijamii kupata wateja kunaweza kusababisha kampuni ipate wateja wengi na kufanikiwa, wawekezaji na washauri wanaweza kuisaidia kampuni ifanikiwe.

Kujitolea

Ni muhimu kwa wahusika wa kampuni au biashara inayoanza kujitolea ili kufikia malengo. Kama kiongozi atajitolea na kufanya kazi kwa juhudi itakuwa rahisi hata kwa wafanyakazi kufanya hivyo.

Uvumilivu

Kampuni zilizofanikiwa zilipitia vikwazo vingi lakini kwa sababu ya uvumilivu zikafanikiwa. Ili kufikia malengo, uvumilivu wa hali ya juu unatakiwa ili kufikia malengo ya kuanzisha biashara husika. haitokuwa rahisi lakini ni muhimu kujikumbusha malengo ili kusonga mbele.

Mabadiliko

Ili kufanikiwa katika biashara inayoanza ni muhimu kutoogopa mabadiliko. Kiongozi anayejua kufanya maamuzi mazuri ikiwa mambo hayaendi kama ilivyopangwa ni dhahiri anaweza kufaidisha kampuni na fursa mpya zinazoweza kujitokeza kabla ya washindani wake.

Wawekezaji

Fedha ni jambo la msingi kwenye biashara. Bila fedha za kuanzia biashara hakuna lolote litakaloweza kufanyika. Viongozi wenye ujuzi hutumia mbinu mbalimbali kutengeneza na kukuza mtaji ili kuweza kukamilisha wazo kwa vitendo.

Ujasiri

Bila ujasiri kampuni inayoanza haiwezi kufika mbali. Kutakuwa na vikwazo vingi lakini ili kampuni iweze kufanikiwa wamiliki wanatakiwa kuwa jasiri na kujikumbusha malengo yao hii itasidia kuwapa nguvu ya kuendelea kupambana.

Muda

Suala la usimamizi wa muda wa ufanisi linatakiwa kuzingatiwa ili kufanikiwa katika kampuni inayoanza. Hivyo ni vyema kwa viongozi wa kampuni husika kutumia vizuri muda wao ili kuweza kufanikiwa.

Utekelezaji husababisha mafanikio kwa sababu kila mtu anaweza kuwa na mawazo yanayoweza kuleta maendeleo makubwa lakini usipokuwa na mkakati wa kuweza kutengeneza wazo kwa matendo, wazo litabaki kuwa wazo tu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter