Mkoa wa dar es salaam umekamilisha agizo la rais Magufuli la kugawa vitambulisho bure kwa wafanyabiashara wadogowadogo (wamachinga) baada ya kugawa vitambulisho vyote 25000 vilivyotolewa katika awamu ya kwanza.
Zoezi hilo la ugawaji vitambulisho limekamilika rasmi januari 3,mwaka huu na kuufanya mkoa wa dar es salaam kuwa wa kwanza kumaliza kugawa vitambulisho hivyo vilivyogawiwa katika wilaya zote tano zinaunda mkoa huo.
Baada ya kukamilisha zoezi hilo kwa ufanisi mkubwa,mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alimuomba Rais Magufuli kumuongezea vitambulisho ombi ambalo lilikubaliwa na kuufanya mkoa wa Dar es salaam kuingia katika awamu ya pili ya ugawaji vitambulisho itakayoanza January 8,2019
Licha ya kumshukuru Rais Magufuli,Makonda pia amesisitiza wafanyabishara kujitokeza kwa wingi kuchukua vitambulisho hivyo ambavyo vitapatikana bure japo wafanyabishara watachangia shilingi 20000 kwa ajili ya gharama za matengenezo ya vitambulisho hivyo.