Home BIASHARABIASHARA NDOGO NDOGO Waonywa kutoza ushuru chini ya tani moja

Waonywa kutoza ushuru chini ya tani moja

0 comment 115 views

Wataalamu na wasimamizi wa mageti katika Halmashauri wametakiwa kuacha kutoza ushuru wakulima wanaosafirisha mazao chini ya tani moja ndani ya Halmashauri husika na kufuata utaratibu wa kiwango cha kutozo kisichozidi asilimia tatu ya mazao yaliyo chini ya Tani moja kwenda nje Halmashauri.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Festo Dugange.

Dkt. Dugange ametoa maelekezo hayo Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu, wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Kilombero Abubakar Damian Asenga aliyehoji je kwanini wananchi wa Wilaya ya Kilombero wanatozwa ushuru wa mazao chini ya tani moja katika geti la Idete, Kivukoni na Kidatu kinyume na maelekezo ya Serikali.

Akijibu swali hilo Dkt Dugange amesema “ni kosa na uvunjifu wa sheria kwa watalaamu au wasimamizi kutoza ushuru kwa wakulima wa ndani ya Halmashauri wanaosafirisha mazao chini ya tani moja ndani ya Halmashauri na tutachukua hatua za kinidhamu kwa yeyote atakayebainika kufanya hivyo.”

Aidha Dkt. Dugange amezielekeza Halmashauri zote nchini kutowatoza ushuru wakulima wa kawaida wa ndani ya Halmashauri wanaotoa mazoa yao shambani kupeleka nyumbani.

Amesema hayo akijibu swali la nyongeza la Mbunge la Jimbo la Bukene Suleimani Zedi aliyetaka kujua, kama Serikali ipo tayari kutoa katazo kwa wataalamu watoza ushuru waache kuwatoza ushuru wakulima wa kawaida ambao sio wafanyabiashara.

“Sheria ya ushuru wa mazao inaeleza wazi kwamba ni marufuku na haitakiwi kutoza ushuru kwa wakulima wakawaida ambao wanatoa mazao yao shambani na kurudisha nyumbani ndani ya Halmashauri,” amebainisha Dkt. Dugange.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter