Home BIASHARABIASHARA NDOGO NDOGO Halmashauri yatimua wafanyabiashara

Halmashauri yatimua wafanyabiashara

0 comment 193 views

Baada ya wafanyabiashara mkabala na Chuo cha Biashara (CBE) Dodoma kutolipa kodi kwa zaidi ya miaka kumi na tano, Halmashauri ya jiji hilo imeendesha zoezi la kubomoa vibanda vyao wakidai kuwa eneo hilo linamilikiwa kihalali na jiji.

Mhandisi wa halmashauri hiyo ambae pia alikuwa akisimamia zoezi la bomoa bomoa Ally Bena ameeleza kuwa wameamua kufanya hivyo baada ya wafanyabiashara hao kukaidi agizo la kulipa kodi. Mhandisi huyo amedai kuwa jiji linaweza kutumia eneo hilo kwa shughuli nyingine za uwekezaji.

Wakizungumzia bomoa bomoa hiyo, baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa wakiendesha shughuli zao za kila siku katika eneo hilo wamedai kushangazwa na zoezi hili kwani hawakuwa na taarifa yoyote. Wameiomba serikali kuwatafutia eneo lingine ili waweze kuendelea na biashara zao.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter