Home FEDHAHISA NICOL yarejea Soko la Hisa

NICOL yarejea Soko la Hisa

0 comment 103 views

Kampuni ya taifa ya uwekezaji (NICOL) imejiunga tena na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) baada ya kuwa nje kwa miaka nane.

NICOL iliondolewa baada ya kukiuka utaratibu wa kujiorodhesha sokoni hapo ikiwemo kushindwa kuonyesha taarifa za fedha na mwenendo wa biashara zilizowekeza. Kampuni hiyo imerudi rasmi DSE baada ya kurekebisha mapungufu yake mwaka jana kwa kuonyesha taarifa zake za fedha na kwa mara ya kwanza kuwalipa wanahisa wake gawio la Sh. 25.

Kwa majibu wa NICOL, thamani ya hisa yake kwa sasa itakua Sh. 300 ambayo iko juu ikilinganishwa na Sh. 270 mwaka 2011 wakati inaondolewa sokoni. Bei ya hisa ya NICOL kwa sasa bado ni ndogo ikilinganishwa na bei yake ya kwanza Sh. 400 mnamo mwaka 2008 wakati inajiunga na Soko la Hisa kwa mara ya kwanza.

Mwaka 2016, NICOL ilitangaza faida baada ya kodi ya kiasi cha Sh. 8.67 bilioni. Thamani ya mali za kampuni iliongezeka hadi kufikia Sh. 94 bilioni kutoka Sh. 23.4 bilioni mwaka 2010. NICOL ina hisa asilimia 6.6 katika benki ya NMB na pia inamiliki asilimia 51 katika kampuni ya ranchi ya taifa.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter