Home BIASHARA Zingatia haya kukuza biashara yako

Zingatia haya kukuza biashara yako

0 comment 1.1K views

Biashara ya nguo ni miongoni mwa biashara ambazo mfanyabiashara anakuwa na uhakika wa kupata wateja kwa sababu mavazi ni moja ya mahitaji muhimu kwa binadamu. Ieleweke kuwa kuna watu wamepata mafanikio makubwa kupitia biashara hii.

Hivyo ni vyema kuangalia mapungufu yaliyopo katika biashara hii na kuyafanyia kazi, ikiwa unataka kufanya biashara ya nguo. Kwa sababu tayari maduka ya nguo yapo kitu ambacho si kibaya, Lakini maduka yote yana bidhaa za watu mbalimbali? Ukipata jibu basi itakuwa rahisi kujua unataka kuuza nguo za aina gani, kwa watu wa aina gani, na umri gani.

Bajeti

Kuwa na mtaji ni muhimu kwa sababu huwezi kuuza nguo kama huna fedha ya kununulia mzigo. Siku hizi mitandao ya kijamii imewarahisishia sana wajasiriamali na wafanyabiashara.

Kuna wafanyabiashara wengi wanauza nguo lakini hawana maeneo ya biashara hivyo wanachokifanya ni kununua mzigo, kuweka nyumbani na kupiga picha ambazo hutumwa katika mitandao ya kijamii mbalimbali ikiwemo Facebook, Instagram, WhatsApp na mingine ili wateja waweze kuona na kununua.

Kulingana na bajeti yako unatakiwa kuamua aidha kama unataka kukodisha eneo (kuwa makini hapa), au utauzia nyumbani kupitia mitandao ya kijamii. Jambo la muhimu ni kuhakikisha unajua wapi utapata fedha au kama utahitaji watu kuwekeza.

Kuwa mbunifu

Suala la uuzaji wa nguo linahitaji mtu mbunifu. Mtu ambaye anaweza kupangilia nguo vizuri ili iwe rahisi kuwahudumia wateja na kuwapa ushauri ikiwa hawajui nini wanahitaji.

Unaweza kuanzisha mitindo yako lakini hakikisha inaendana na mitindo mingine ya kisasa ili kuwahamasisha watu kuja kununua zaidi na vilevile kujitengenezea jina.

Pangilia vizuri biashara yako

Kama utapata eneo basi hakikisha muonekano wa duka lako unawavutia wateja, usafi ni muhimu. Kama utatumia mitandao basi hakikisha akaunti yako ina picha au video zinazovutia ili wateja wahamasike kununua bidhaa zako, unatakiwa kuwa mkweli usiweke vitu ambavyo havipo mitandaoni kwa kufanya hivyo unaweza kupoteza wateja na kupunguza uaminifu.

Hakikisha umepanga mpango wa kutafuta masoko kabla hujaanza biashara yako. Unaweza kutengeneza tovuti, kuongea na watu wengine wenye tovuti ili uweze kutangaza biashara yako, unaweza kutumia mitandao mbalimbali kutangaza biashara lengo ni kupata wateja wengi.

Aidha watu wanapenda vitu vizuri kwa bei nafuu hivyo weka bei zinazoendana na bidhaa husika ili kuwavutia wateja wengi. Pia jitahidi kufanya punguzo la bei ili kuwahamasisha watu wengi.

Vilevile jenga uhusiano mzuri na wateja wako ili watangaze biashara na huduma yako kwa ujumla.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter