Home FEDHA Mfumo wa huduma za kifedha bado tatizo

Mfumo wa huduma za kifedha bado tatizo

0 comment 36 views

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Taasisi ya kuendeleza huduma za kifedha Tanzania (FSDT) Irene Mlola amesema takribani asilimia 28 ya watanzania wenye umri kuanzia miaka 16 na kuendelea wapo nje ya mfumo wa huduma za kifedha. Mlola amesema hayo katika kikao cha utekelezaji wa sera ya taifa ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2017 wakati akiwasilisha mada ya mchango wa ubunifu katika kufikisha huduma ndogo za fedha. Katika maelezo yake, Mkurugenzi huyo amedai kuwa idadi ya watanzania waliokuwa nje ya mfumo wa kifedha ilikuwa asilimia 55 mwaka 2009, asilimia 27 mwaka 2013 na asilimia 28 mwaka 2017.

Sera hiyo inatazamwa kuleta Sheria na kanuni ambazo zitawafikia watu wengi zaidi huku ikiweka mbele masuala ya matumizi ya teknolojia na mifumo jumuishi ili kupata huduma zenye ubora.

“Kwa waliopo kwenye mfumo wa kifedha kwa mwaka 2009 ni asilimia 9, mwaka 2013 ni asilimia 14 na mwaka 2017 ni asilimia 16.7”. Ameeleza Mlola.

Vilevile, Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa ubunifu katika teknolojia ya mitandao na mifumo ya jamii umefanikiwa kufikiwa kwa walaji wengi kwa kiasi kikubwa huku akisisitiza kuwa ubunifu unatakiwa ili kuwavuta watanzania asilimia 28 waliopo nje ya mfumo kwa sasa.

Mlola pia amechukua fursa hiyo kuzungumzia idadi kubwa ya watanzania hutafuta huduma za kifedha kwenye sekta ndogo kama vile Saccos, Vicoba na vikundi licha ya kwamba sekta hizo zimekuwa na changamoto ya usimamazi kwa muda mrefu. Mkurugenzi huyo amesisitiza kuwa changamoto hizo zitatatuliwa kupitia sera hiyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter