Serikali ya Tanzania imesema tangu makato ya tozo yaanze kwa kipindi cha wiki 4 imekusanya zaidi ya Bilioni 48 kupitia tozo za miamala ya simu.
Zaidi ya Bilioni 22 tayari zimepelekwa kwenye maeneo ambayo hayana vituo vya afya (zaidi ya vituo 90), na Agosti 19, 2021 zaidi ya Bil 15 zimepelekwa kwenye eneo hilohilo na kufanya vituo kuwa zaidi ya 150.
Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia tozo hizo zilizotangazwa hivi karibuni.
Soma zaidi: Tozo za miamala zamfikia Rais Samia
Amesema “kati ya hizi zaidi ya Tsh. Bil 48 tulizokusanya kwenye makato ya tozo kwa hizi wiki nne, zaidi ya Bil 7 zimepelekwa kwenye madarasa, mtaona wenyewe tumepeleka fedha zijenge vituo 150 ambavyo vinaokoa maisha yetu, pia madarasa zaidi ya 500, ni Watoto wetu wanasoma”
“Ndani ya wiki hizo nne za makato kwenye miamala kwa miezi hii minne kwa upande wa Zanzibar wamekusanya Bilion 1.6, kwa hiyo utaona jambo hili lina matokeo” Amesema Nchemba.