Home BIASHARA TPDC,Dangote waingia mkataba

TPDC,Dangote waingia mkataba

0 comment 37 views

Shirika la Taifa la Maendeleo ya Petroli (TPDC) limeingia mkataba wa kuuza gesi asilia kwa kampuni ya Dangote Tanzania ili kusaidia kiwanda hicho kutumia gesi katika uzalishaji wake. Makubaliano hayo yanatarajia kuongeza kiwango cha uzalishaji wa umeme kutoka MW 20 hadi MW 35.

Akizungumzia makubaliano hayo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha Dangote, Jagat Rathee amesema makubaliano hayo yatasaidia kiwanda hicho kuongeza uzalishaji kutokana na matumizi ya gesi kuwa nafuu kuliko yale ya Dizeli ambapo siku za nyuma, kwa wastani, kiwanda hicho kililazimika kutumia lita 106,000 za mafuta hayo kwa siku kuzalisha tani 2,000 za saruji.

Naye Kaimu Mtendaji wa TPDC Kapuuly Musomba amesema kiwanda cha Dangote ni miongoni mwa viwanda saba vilivyopo kwenye mpango wa shirika hilo kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

“Tunafahamu kwamba serikali iko katika hatua za kujenga uchumi wa viwanda, hivyo sisi (TPDC) kwa nafasi yetu tumejipanga kuhakikisha viwanda vinazalisha bidhaa kwa gharama nafuu kupitia matumizi ya gesi asilia”. Amesema Musomba.

Kusimama kwa uzalishaji katika kiwanda hicho kutokana na matatizo ya nishati kumechangia kwa kiasi kikubwa kupanda kwa bei ya saruji kutoka Sh. 12,000 hadi Sh. 18,000.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter