Home BIASHARA Ma-Rc wapokea Vitambulisho vipya

Ma-Rc wapokea Vitambulisho vipya

0 comment 135 views

Wakuu wa mikoa yote nchini wamepokea vitambulisho 1,100000 kwa mara ya pili maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara wadogowadogo (wamachinga) jana ikulu jijini Dar es salaam.

Vitambulisho hivyo vilitolewa na katibu mkuu kiongozi Balozi John Kijazi baada ya wakuu hao awali kupokea vitambulisho 25000 kwa kila mkoa ikiwa ni mpango wa serikali ya awamu ya tano kuongeza mapato na kuboresha mazingira ya kufanyia biashara kwa wajasiriamali hao nchini.

Katika awamu hii ya pili kila mkoa ulipata idadi tofauti kulingana na mahitaji tofauti na hapo awali,Mkoa wa dar es salaam uliongoza kwa kupata vitambulisho 150000 ukifuatiwa na arusha uliopata vitambulisho 100000 huku mbeya wakipata 80000 na mwanza 55000,Mikoa mingine ilipata idadi ya chini huku baadhi ya mikoa ikifungana kwa idadi.

Vitambulisho hivyo huuzwa kwa wamachinga kwa bei elekezi ya shilingi 20000 na vimetengenezwa maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara ambao mtaji wao hauzidi shilingi milioni nne.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter